LULU AMUOMBA MUNGU AFANIKISHE NDOA YAKE

0
1146

Na BRIGHITER MASAKI


MSANII wa Filamu nchini, Elizabeth Michael (Lulu), amesema yupo katika maombi ili aweze kuolewa kama alivyopanga.

Lulu alisema hayo alipokuwa kwenye sherehe za harusi ya msanii wa muziki wa Bongo Fleva na Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule (Profesa Jay), iliyofanyika juzi kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

“Namuomba Mungu anipiganie kwenye uhusiano wangu ili niweze kutimiza lengo langu la ndoa na mtu niliyenaye kwenye uhusiano wa kimapenzi.

“Ndoa ni jambo la kutokea kati ya makubaliano yetu hivyo siku nikiolewa nitakachotoa kama zawadi kwa mashabiki wangu ni uhuru wa kuniuliza chochote watakacho na nitawajibu,” alieleza Lulu aliyekuwa amevalia vyema gauni lake.

Licha ya kueleza hayo Lulu hakuwa tayari kumtaja wala kumzungumzia mpenzi wake wa sasa.

“Sipo tayari kuzungumzia kitu kinachohusu mahusiano yangu kwa sasa, tukijijua wenyewe inatosha, wengine watajua mpaka siku ya ndoa yangu ambapo nitajibu na kuzungumzia mambo yote mnayotaka kujua kuhusiana na uhusiano wangu maana vitu vya ndoa vinakujaga tu, namuomba Mungu azidi kunipigania na kunipangia malengo yangu ya ndoa na kuwa na familia yatimie,” alisema Lulu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here