23.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

LUKUVI NJOO UTUSAIDIE MGOGORO WA ARDHI-WITO

NA RAYMOND MINJA IRINGA


William LukuviBAADHI wananchi, akiwemo Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kidete katika Kijiji cha Mgera wilayani Iringa,  wamemuomba Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo  Makazi, William Lukuvi  kuingilia kati mgogoro wa aridhi unaotaka kuzalishwa na serekali ya kijiji kwa kuwalazimisha wananchi wake kutoa maeneo yao kwa mwekezaji bila ya idhini yao .

Hatua hiyo, imekekuja baada ya Taasisi ya Ngoti Green Hills Estate Foundation, kuhitaji zaidi ya ekari 40 katika kitongoji hicho kwa ajili ya uwekezaji binafsi wa hospitali, kituo cha watoto yatima na chuo cha ufundi.

Baadhi ya wananchi, akiwamo mwenyekiti wa kitongoji hicho, Victor Malila wamepinga mpango wa mwekezaji huo kununua ardhi inayomilikiwa na wananchi kwa bei anayotaka yeye.

Malila, alisema wengi wao wameishi maisha yao yote kwa kutegemea ardhi hiyo, inayowapatia chakula na kipato kutokana na shughuli mbalimbali za kilimo.

Alisema ni vema Serikali ikaingilia kati jambo hilo, kuna wanachi wanataka kupokwa aridhi yao  na mwekezaji tena anayetaka kununua maeneo hayo kwa bei ya kutupwa wakati watu waliendeleza maeneo hayo kwa garama kubwa

Mmoja wa wapingaji wa mpango huo, Augustino Ngao alisema hawezi kuuza  ekari zake zaidi ya nne kwa mwekezaji huyo kwa sababu zimekuwa zikimpatia zaidi ya magunia 100 za mahindi na 50 za maharage kila mwaka.

Kaimu Ofisa Ardhi wa Wilaya ya Iringa, Geofrey Kaluwa alisema sheria za ardhi hazimpi mamlaka mwekezaji binafsi kuchukua  ardhi ya wananchi bila kukubaliana nao, mmoja mmoja au kwa pamoja, kwa kuwa kinachotaka kuwekezwa hapo hakiwi cha umma.

Naye Mkurugenzi wa Ngoti Green Hills Estate Foundation, Thomas Ngoti alijitetea akisema amefuata taratibu zote muhimu zinazotakiwa ili kuipata ardhi hiyo.

Alisema aliomba eneo hilo,baada ya kuelezwa na Serikali ya kijiji kwamba haina eneo analoweza kuuziwa na badala yake aombe maeneo ya wananchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles