27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

LUKUVI: MARUFUKU KAMPUNI ZA KUPIMA ARDHI KUDAI WANANCHI

Maregesi Paul, Dodoma

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amepiga marufuku makampuni yanayopima ardhi yasiwadai wananchi gharama za upimaji wa ardhi.

Amesema kila makampuni hayo yatakapokuwa yakipima ardhi yatatakiwa kulipwa fedha za upimaji kupitia kwenye vikundi vilivyochaguliwa na wananchi.

Lukuvi ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma leo, alipokuwa akiwasilisha bajeti ya Wizara yake kwa Mwaka wa Fedha 2018/19.

“Aidha, wapimaji hao wanatakiwa kutoa taarifa katika uongozi wa wilaya husika kuhusu uwepo wao katika maeneo wanayopima ardhi,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, Waziri Lukuvi aliwahimiza wananchi kuwa na kawaida ya kulipa kodi ya ardhi kila mwaka kwa kuwa ni wajibu wao kisheria.

“Kwa upande wa wananchi wanaokabiliwa na migogoro ya ardhi, nawaomba wafike kwa maofisa wa wizara yangu ili migogoro yao iweze kutatuliwa haraka iwezekanavyo,” amesema Lukuvi.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles