29.3 C
Dar es Salaam
Friday, September 20, 2024

Contact us: [email protected]

Lukuvi asimamisha wawili, ateua 20

Na RAMADHAN HASSAN

DODOMA

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amemwagiza Katibu Mkuu  wa Wizara hiyo, Dorothy Mwanyika awasimamishe kazi wenyeviti wa wawili wa mabaraza ya ardhi huku akiteua wengine 20.

Akizungumza jana na waandishi wa habari alisema wizara imeunda mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya 97 kwa ajili ya kushughulikia utatuzi wa migogoro ya ardhi kwa mujibu wa sheria ya mahakama na utatuzi wa migogoro ya ardhi sura 216.

“Nimekuwa nikipokea tuhuma kuhusu utendaji wa wenyeviti wa mabaraza  ya ardhi na nyumba ya wilaya hususani mabaraza ya wilaya ya Karagwe na Kibaha,

“Kwa mamlaka niliyonayo namwagiza Katibu Mkuu kuanzia leo (jana), kuwasimamisha kazi wafuatao ili kupisha uchunguzi,” alisema.

Waliosimamishwa ni Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya ya Karagwe, Rugate Assey na Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya ya Kibaha, Jerome Njiwa.

“Tuhuma ni kwamba wamelalamikiwa na watu wengi kwamba wanapokea rushwa,”alisema Waziri Lukuvi.

Katika hatua nyingine Lukuvi amewateua wenyeviti 20 wa mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya wilaya kwa kipindi cha miaka mitatu.

Lukuvi alisema mamlaka aliyonayo yanampa nafasi ya kuwateua wenyeviti hao pale anapoona inafaa.

“Nimewateua wenyeviti 20 wa mabaraza ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ya Wilaya kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia Aprili moja mwaka huu” alisema Lukuvi.

Aliwataja wateule hao kuwa ni Rajabu Mnyukwa, Edward Muhina, Nadhiru Ngukulike, Rebeca Mjanja, Hussein Lukeha, Augustine Lugome, Baraka Shuma, Tendai Chinolo, Mangeti Sangiwa, Jackson Kanyerinyeri, Jacob Kabisa, Ntumengwa Moses, Justine Lwezaura, Jesca Mugalu, Regularly Mtei, Jimson Mwankenja, Bahati Ndambo, Richard Mmbando, Felix Rutajangulwa na Ngasa Masunga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles