28.7 C
Dar es Salaam
Monday, October 25, 2021

LUKUVI AGAWA HATI 122 SIMIYU

Na Mwandishi Wetu-SIMIYU


WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amegawa hatimiliki za ardhi 122 kwa wananchi wa Lamadi, mkoani Simiyu wakati alipofanya ziara yake mikoa ya Kanda ya Ziwa, kuhamasisha ulipaji kodi ya pango la ardhi na suala la urasimishaji wa makazi holela.

Wananchi hao 122 ni wale waliofanikiwa kulipia michango yote, hivyo kuondokana na makazi holela na kuishi katika makazi rasmi.

Hata hivyo, jumla ya wananchi 5,200 wa Lamadi Mkoa wa Simiyu washapimiwa maeneo yao kwa urasimishaji, na watapatiwa hati zao mara tu baada ya kukamilisha michango stahili.

Katika ziara hiyo, Waziri Lukuvi alifika Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza na kufanya ukaguzi wa mfumo wa ulipaji kodi ya pango la ardhi wilayani hapo na kugundua kati ya wakazi 35,000 wanaotakiwa kulipa kodi ya ardhi, 28,000 wameishapelekewa hati ya madai.

Mbali na hili, Waziri Lukuvi, alitembelea Idara ya Ardhi ya wilayani Nyamagana na kukagua mafaili ya kumbukumbu za wananchi, kuhusu taarifa za ardhi ikiwamo masuala ya hati na kugundua baadhi ya viongozi hawajalipa kodi ya pango la ardhi.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,099FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles