33.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 29, 2024

Contact us: [email protected]

Lugola: Viongozi msitumie dini kujificha

Felix Mwagara, MOHA-Ngara

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema baadhi ya viongozi wa dini wamejipenyeza na kuanzisha makanisa na misikiti kwa lengo la kuanzisha vichaka vya kujificha ili tujue ni watu wa Mungu kumbe wanataka kufanya uchochezi na kuvuruga amani.

Lugola alisema Serikali haitawavumilia wale wote walioanzisha taasisi hizo kwa lengo lao binafsi na itahakikisha inawashughulikia ipasavyo bila kuwaonea huruma.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na mamia ya wananchi wa mji wa Ngara  kuwa makanisa na misikiti ambayo imesajiliwa na wizara yake hatakubali kuona viongozi hao ambao wanajifanya kuwa na watu wa Mungu kumbe wanamalengo hayo binafsi.

“Makanisa na miskiti itakayobainika ina malengo hayo, sitaona haya kuifutia usajili, nawataka viongozi wa dini endapo migogoro inaibuka hakikisheni  mnaitatua wenyewe kwa amani,” alisema Lugola.

Waziri Lugola alisema Serikali inaheshimu imani ya dini na pia viongozi wao wanamchango mkubwa katika maendeleo ya nchi kutokakana na maombi pamoja na kuwaongoza waumini wao vizuri, lakini pia wapo baadhi ya viongozi hao wa dini, wanaingiza masuala ya siasa makanisani na misikitini.

“Niwaomba viongozi wote wa dini, wakati tunapoenda katika uchaguzi, viongozi wa makanisa na misikiti iliyosajiliwa, niwaombe pale migogoro inapoibuka hakikisheni mnaitatua wenyewe kwa amani na msiruhusu mtu ambaye ana nia mbaya na maendeleo ya nchi hii, aje kuwaingilia,” alisema Lugola.

Katika mkutano huo, aliitaka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), ipitie upya usajili na utoaji wa vitambulisho vya taifa katika mikoa ya Kagera na Kigoma ili kuwabaini  na kuwaondoa raia wa nchi jirani zinazoizunguka mikoa hiyo.

Alimpa wiki mbili  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji,Dk. Aana Makalala  awe amefika katika mikoa hiyo kwa ajili ya kuanza maandalizi ya kufanya operesheni kubwa ya kuwaondoa wahamiaji haramu katika mikoa hiyo kabla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kuanza Julai, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles