28.6 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

LUGOLA AWATOA MKUTANO MAKAMANDA ZIMAMOTO

Na SARAH MOSES-DODOMA


WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewatoa nje makamanda zaidi ya 30 kwa   kutotaja kwa ukamilifu Jeshi la Zimamoto  huku wakishindwa kutaja neno Uokoaji.

Alisema  hiyo ni dalili kwa viongozi hao wa jeshi hilo kufanyakazi kwa mazoea na kutojua misingi ya jeshi lao hasa kwenye uokoaji.

Hali hiyo ilijitokeza   Dodoma jana kwenye ufunguzi wa kikao cha mwaka cha Makamanda wa Zimamoto na Uokoaji ambako alisema  makamanda hao wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea.

Alisema   yeye analijua Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na wale wote ambao walijitambulisha bila kumalizia na uokoaji watoke nje.

“Nisikilizeni kwa makini makamanda ambao nimewaita majina yenu simameni na ambao hamjasikia nikitaja majina yenu tokeni nje kwa sababu  jeshi lenu mlilolitaja silitambui hivyo kikao hiki hakiwahusu.

“Haiwezekani ofisa mzima unasimama unajitambulisha kuwa unatoka Jeshi la Zimamoto, kwa hiyo kazi yenu nyinyi ni kuzima moto tu na siyo pamoja na uokoaji,” alisema Lugola.

“Kamishna Jenerali nenda ukalisimamie jambo hili kwani naona bado linajirudia, pia wengine wamejitambulisha hapa sauti zao hazina mpangilio  wakati sauti inaweza kufundishwa kwa siku mbili tu.

“Vilevile mtu akiwa mnyonge hata  saluti hawezi kuipiga wakati kuna namna ya kukata mkono wa saluti,”alisema Lugola.

Alisema ameshtushwa na taarifa iliyotolewa na Kamishina Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye kuwa mamlaka za maji zimekuwa zikililipisha  jeshi hilo fedha kutokana na maji wanayotumia kwenda kutoa huduma ya bure kwa wananchi wanaofikwa na majanga ya moto.

“Nimeshitushwa na taarifa hii kwa sababu  hivi karibuni nilizungumza na baadhi ya wakurugenzi wa mamlaka za maji ambao walisema   hawalitozi gharama Jeshi la Zimamoto,”alisema.

Lugola alisema Jeshi la Zimamoto halitakiwi kudaiwa fedha za maji kwa vile  linafanya kazi ya kuhudumia wananchi bure.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles