31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Lugola atoa maagizo mengine kwa IGP

Na PENDO FUNDISHA-MBEYA

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, amemuagiza Inspekta Jenerali wa Polisi, IGP, Simon Sirro, kupunguza vituo vya ukaguzi wa magari barabarani  kupunguza vitendo vya rushwa kwa askari wasio waadilifu.

Lugola, ambaye yupo mkoani Mbeya kufuatilia maagizo aliyotoa   alivyoteuliwa, alisema baada ya Serikali kuongeza nguvu na kuweka mikakati ya udhibiti wa ajali barabarani, baadhi ya askari wa usalama barabarani ambao si waadilifu wameamua kutumia njia hiyo kama fursa ya kujipatia fedha.

“Nafahamu tumejipanga kudhibiti matukio ya ajali zinazosabisha vifo vya watu wengi, lakini mikakati hii isiwe ni sehemu ya kuumizana.

“Wapo askari wameamua kugeuza mikakati hii kuwa ni vitegauchumi, tafadhali sana naliomba hili likomeshwe,”alisema.

Alisema amekuwa akipigiwa simu na kupata taarifa juu ya vitendo vya rushwa vinavyoendeshwa na baadhi ya askari wa usalama barabani.

Waziri alisema kwa sababu hiyo  ni vema IGP akaliona hilo na kuangalia njia mbadala itakayosaidia kupunguza vitendo hivyo ambavyo vinaliletea jeshi la polisi picha mbaya.

“Vituo vya ukaguzi vipo karibu karibu mno, unakuta kila hatua 20 kuna kituo, hili ni tatizo jamani, lazima tuliangalie hili.

“Fursa ziwe na manufaa kwa watu wote si baadhi, vituo hivi vimekuwa vikiwapotezea watu muda,”alisema.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, alimuomba Lugola kumfikishia maombi yake kwa rais ya kuongezewa vitendea kazi yakiwamo magari ya washa washa.

Alisema Jimbo la Mbeya Mjini lina kata zaidi ya 36 na magari ya polisi ni machache   hivyo wanahitaji magari mengine ya ziada.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei, alimuomba Waziri   Lugola, kuwaongezea vifaa vya upimaji wa ulevi kwa madereva  kwa vile  vilivyopo havikidhi mahitaji.

“Vifaa vya upimaji wa ulevi wa pombe kwa madereva ni vichache na ukiangalia kila kifaa kimoja kikitumika hakitumiki tena, hivyo mahitaji ni makubwa,  tunaomba suala hili lipewe kipaumbele,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles