27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 4, 2023

Contact us: [email protected]

Lugola afukuza viongozi polisi wilaya nzima

Mwandishi Wetu-Nkasi

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amewaondoa katika nyadhifa zao viongozi wakuu wa Jeshi la Polisi wa Wilaya ya Nkasi, mkoani Rukwa kwa kushindwa kumudu majukumu yao baada ya kubaini kuwepo kwa wizi wa mara kwa mara wa mifugo wilayani humo.

Lugola pia ameagiza askari sita wa Kituo cha Polisi Namanyere na Kirando wilayani humo waondolewe kutokana na wananchi kuwalalamikia kwa kushindwa kuwasaidia wanaporipoti matukio mbalimbali. 

Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara, mjini Namanyere, Lugola alisema Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD), David Mtasya, Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya (OC CID), Emanuely Kajala na Mkuu wa Kituo cha Polisi Namanyere (OCS) wilayani humo, Ramadhani Msangi, lazima waondoke katika wilaya hiyo kwa kuwa wameshindwa kuimudu kazi yao ipasavyo.

“Kufuatia malalamiko yaliyowasilishwa mkutanoni hapa kama mlivyowasikia, wananchi hawapati msaada kutoka kwa Jeshi la Polisi wanalipotoa taarifa ya kuibiwa ng’ombe, wameibiwa ng’ombe 278 wanatoa taarifa kwenye kituo cha polisi lakini hawasikilizwi.

“Wanazungushwa, wanapuuzwa mpaka kiasi kikubwa cha ng’ombe kimepotea, licha ya kuwa wananchi 15 waliripoti polisi, mpaka sasa hawajapata msaada wa polisi, hii haiwezekani na siwezi kukaa kimya, viongozi hawa wameshindwa kazi, lazima waondoke waje wengine,” alisema Lugola.

Alisema licha ya polisi hao kupokea malalamiko mengi vituoni, wanawaachia watuhumiwa mitaani kiasi kwamba wananchi wanapatwa na hasira na kuanza kuichukia Serikali.

Mkazi wa Namanyere wilayani Nkasi, Felista Mkomo, alisema mwaja jana aliibiwa ng’ombe wake lakini walifanikiwa kuwakamata wawili ila wengine mpaka sasa hawajawapata, hata hivyo aliripoti tukio hilo kituo cha polisi lakini mpaka sasa hakuna kilichofanyika.

“Mimi kero yangu ni wizi wa ng’ombe, niliibiwa mwaka jana, katika kuwatafuta nikafanikiwa kuwapata wawili, nikaamua kwenda polisi kuripoti tukio hili la wizi, mpaka sasa hakuna taarifa zozote na sijawapata ng’ombe wangu,” alisema Felista.

Waziri Lugola akijibu kero hizo, alisema Serikali ya Dk. John Magufuli haiwezi kuchezewa na mtu yeyote, na kamwe haiwezi kuona wananchi wake wanateseka kiasi hicho.

Aidha Polisi mkoani humo, kuwasaka wazazi na walezi ambao wanawatumikisha watoto wao kufanya kazi katika ziwa Tanganyika badala ya kuwapeleka shule na kuendelezea wimbi la umaskini. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles