23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

LUGHA YA KIINGEREZA KIKWAZO WANAFUNZI WA SEKONDARI

NA MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM


KWA muda mrefu sasa kumekuwepo na mijadala mbalimbali ya wadau wa elimu nchini, wakilalamikia Tanzania kutokuwa na sera rasmi ya kutumika lugha ya Kiingereza pekee kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu.

Kutokona na kutokuwapo na sera hii, wanafunzi hususani wa shule za serikali hukutana na lugha ya Kiingereza kama somo la kufundishia mara wafikapo sekondari jambo ambalo huwachanganya walio wengi.

Shuhuda mbalimbali zilizotolewa na wadau wa elimu na wanafunzi wenyewe, zinaonyesha kuwa Tanzania imekuwa ikipoteza wataalam katika nyanja mbalimbali kutokana na kuendelea kukitumia Kiingereza katika masomo ya shule za sekondari tu.

Imeelezwa kuwa kwa kuwa masomo yote katika ngazi ya elimu ya msingi hufundishwa kwa Kiswahili, watoto wanapojiunga na elimu ya sekondari hujikuta wakiambulia patupu katika masomo yao kutokana na kutoielewa lugha ya Kiingereza inayotumika kufundishia.

Ni kutokana na hali hiyo, wadau mbalimbali wamekuwa wakisisitiza umuhimu wa masomo ya sekondari na hata chuo, kufundishwa kwa lugha ya Kiswahili ili wanafunzi waweze kuyaelewa vizuri.

Wadau hao wamekuwa wakitolea mfano kwa nchi kama za China, Urusi na nyinginezo ambazo zinafundisha masomo katika lugha zao na matokeo yake, wanafunzi wamekuwa wakiyaelewa kwa kiasi kikubwa na mwisho wa siku, kuwafanya kuwa wataalamu wa kiwango cha juu katika fani mbalimbali tofauti na na hapa nchini.

Shule ya Sekondari ya Kiislam ya Wasichana ya Kunduchi Girls Islamic High School ya jijini Dar es Salaam ni miongoni mwa wadau wa elimu wanaokumbana na changamoto ya lugha ya kiingeza kwa wanafunzi wao, hasa wa kidato cha kwanza

Katika mahojiano maalum na gazeti hili, Mkuu wa shule hiyo, Khadija Mgambo, anakiri kwamba shule nyingi za sekondari zinapokea wanafunzi ambao hawana misingi mizuri katika kumudu vyema somo la kiingereza, jambo ambalo linaleta ugumu kwa sababu ndiyo lugha kuu ya kufundishia.

“Nikiri kwamba lugha ya kiingereza bado ni tatizo kubwa kwa wanafunzi wetu wanaohitimu darasa la saba. Bado serikali inalo jukumu la kusaidia kuboresha eneo hilo kuanzia shule za msingi ili wanafunzi wanapojiunga na elimu ya sekondari, wawe na uwezo wa kutambua kile wanachojifunza kupitia lugha inayotumika” anasema.

Anasema ili kukabiliana na tatizo wamelazimika kuwa na program mbalimbali za masomo ya dini na lugha ya kufundishia ambapo hutumia muda wa ziada baada ya muda wa masomo ya darasani hu, pamoja na mitihani ya mara kwa mara lengo ni kuwasaidia wanafunzi hao wapya kumudu masomo.

Kuhusu uelewa mdogo kwa wanafunzi wanaohitimu darasa la saba, anasema: “Hii  ni changamoto kwani tunapokea baadhi ya wanafunzi waliohitimu wakiwa na uwezo mdogo ambao kama tukiwaacha itakuwa ngumu kumudu masomo ya sekondari.”

Mgambo anasema hali hiyo ndiyo inasababisha baadhi ya shule binafsi kusajili wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao ya kuhitimu darasa la saba pekee.

“Hata hivyo, Kunduchi Girls Islamic High School wanaona huo ni ubaguzi kwakuwa haki ya kusoma niya kila mtanzania, hivyo wanalazimika kuwapokea  wanafunzi wote bila kubagua huku wale wasio na uwezo zaidi wakianzishiwa program maalum za kuinua viwango vyao vya uelewa.

Shule hiyo ambayo niya bweni inayo miundombinu yote muhimu ya kujifunzia na kufundishia yakiwamo maabara ya sayansi na maktaba za kompyuta ili kuwarahisishia walimu na wanafunzi kupata kilicho bora bila kusahau maadili ya dini ya kislamu na nidhamu ya hali ya juu.

“Kwetu sisi tunajitahidi kuwa na walimu mahiri waliotoka vyuo vikuu wenye uwezo mkubwa zaidi wa kufundisha na kutuletea mafanikio kwa matokeo ya kidato cha nne na cha sita kama yalivyo sasa.

 “Tunafanya tathmini ya namna walimu wanavyofundisha na wanafunzi wanavyopokea maarifa na stadi mbalimbali, haya yamefanyika na kutuletea matunda mazuri yanayoonekana,” anasema mkuu huyo wa shule.

Aidha Mgambo anasema mwanafunzi wa shule hiyo anajengewa kuheshimu taratibu za shule, sheria za nchi na kuwa tayari kujitolea kwa ajili ya taifa na jamii yake kwa ujumla.

“Tunaandaa wanafunzi kuwa wanajamii wanaojiamini ambao pia watakuwa wachangiaji wa maendeleo ya taifa kwa namna moja au nyingine,” anasema mkuu huyo na kuongeza

“Tunajivunia kuwa na wanafunzi katika vyuo vikuu vingi ndani ya nje ya nchi,  taasisi na sehemu nyingi za ajira waliopitia katika shule yetu wameonesha kuwa na nidhamu na kupendwa na wenzao kutokana na misingi mizuri tuliyowajengea kabla ya kuhitimu masomo yao.

Kunduchi Girls Islamic High School ilianzishwa miaka 25 iliyopita kilomita chache kutoka barabaru kuu ya Bagamoyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles