LOWERY ABAKISHA WIKI MOJA KUISHI

0
685

LONDON, ENGLAND


SHABIKI mkubwa wa klabu ya Sunderland ya nchini England, Bradley Lowery, mwenye umri wa miaka sita, amebakisha wiki moja ya kuishi, kutokana na ugonjwa wake wa saratani kusambaa mwilini.

Kupitia ukurasa wa Facebook, mama wa mtoto hiyo, Gemma, aliandika ujumbe kwa hisia kali huku akidai kuwa moyo wake umejigawa sehemu mbili juu ya mtoto wake, ambaye anateseka sana na saratani, huku ugonjwa huo ukionekana kuwasumbua sana watoto nchini Uingereza na inadaiwa kila mwaka watoto zaidi ya 100 wanasumbuliwa na ugonjwa huo.

“Mwanangu Bradley Lowery anateseka sana, katika redio mbalimbali amekuwa akichangiwa fedha ili kuweza kupewa matibabu ya kupunguza maumivu makali ya kwenye mifupa ambayo anayapata mara kwa mara, ni kweli, lakini kwa sasa hali hiyo ya maumivu inaonekana kutokea kile sehemu badala ya kwenye mifupa.

“Juzi alifanyiwa vipimo kwenye kifua, cha kusikitisha ni kwamba amegundulika kuwa saratani inazidi kuenea sehemu kubwa ya mwili wake kwa haraka sana kwa sababu hewa ya oxygen kwenye mapafu ipo kidogo, kwa kuwa sehemu kubwa zimeziba, hivyo hewa hiyo haikai.

“Kwa hali hiyo tumeambiwa kuwa Bradley amebakiwa na wiki moja tu ya kuishi kutokana na saratani kuenea kwa haraka mwilini, ni wazi kwamba moyo wangu sasa umegawanyika sehemu mbili, kwa kuwa ninaona ni mapema sana kwa mwanangu kuondoka.

“Mwanangu ameteseka sana katika kipindi cha miaka minne na bado anazidi kuteseka, lakini bado tunamuombea hadi hatua za mwisho,” aliandika Gemma

Desemba mwaka jana wataalamu walisema hali ya mtoto huyo ni mbaya na angeweza kuishi kwa miezi miwili tangu hapo, lakini hadi sasa Mungu ameendelea kuwa na shabiki huyo kwa miezi sita sasa tangu taarifa hiyo itolewe na sasa wametoa tena.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here