25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Lowassa amwagia sifa Magufuli

Mwandishi Wetu, Monduli

Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, amemmwagia sifa Rais John Magufuli, kuwa ni kiongozi mwenye maono huku akiwataka Watanzania wamuunge mkono.

Lowassa amesema hayo leo Jumamosi Machi 9, Monduli mkoani Manyara, katika mkutano wa kumpokea baada ya kurejea CCM akitokea Chadema alikohamia mwaka 2015.

“Kwa sasa mambo yanakwenda kwa kasi kasi hii anaifanya Rais nimekuja kuwaombeni tumuunge mkono ili kazi hii iendelee vizuri.

“Napenda kuwaambieni Rais Magufuli ni kiongozi anayetazama mbele (Vision Leader), ndiyo maana nchi inakwenda kwa kasi sana inawezekana kukatokea makosa ya hapa na pale lakini nchi inakwenda kwa kasi inayopasa.

“Sina mashaka juu ya uongozi wake na naamini tukimuunga mkono wote kwa pamoja tutafika mbali sana,” amesema Lowassa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles