Texas, Marekani
Baada ya kimya cha muda mrefu, mwongozaji na mwigizaji gwiji wa filamu kutoka Houston Texas Marekani, Alenga Elize maarufu Alenga The Great, amefyatua sinema yake mpya ya Kiswahili inayoitwa ‘Lost Love (Wolf In a Sheep Clothes)’.
Alenga The Great amejizolea umaarufu kwa kuandaa filamu zenye msisimko wa aina yake huku akiing’arisha vyema tasnia ya Bondowood Movie.
Akizungumza na mtanzania.co.tz, Alenga The Great, amesema ndani ya muda mfupi filamu hiyo imefanikiwa kutazamwa na maelfu ya watu katika chaneli yake ya YouTube jambo linalompa moyo wa kuendelee kuipambania tasnia hiyo akiwa nchini Marekani.
“Ni filamu yenye maudhui ya kiafrika, ina visa vya kusisimua, mapenzi ya dhati na usaliti vimetawala na haupaswi kuacha kuitazama filamu hii ambayo tayari ipo kwenye channeli yangu ya YouTube, naishukuru timu yangu nzima ya Izack Productions na waigizaji wote ambao wamevaa uhusika ndani ya Lost Love,” amesema Alenga.
Ameongeza kwa kuwaomba mashabiki kwenda kuitazama filamu hiyo kwenye link https://youtu.be/kUY_PYm48EI?si=rJkcDhzyrHa-04On.