28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Ljungberg awapa Arsenal matumaini ‘Top Four’

LONDON, ENGLAND

KOCHA wa muda wa timu ya Arsenal, Freddie Ljungberg, amesisitiza kuwa bado timu hiyo ina nafasi ya kuingia kwenye nafasi nne za juu bila ya kujali sare ya mabao 2-2 dhidi ya Norwich City.

Hii sio mara ya kwanza kwa Arsenal kuanza vibaya lakini kuja kumaliza nafasi nne za juu kama ilivyokuwa msimu wa mwaka 1975, hivyo kocha huyo anaamini timu hiyo inaweza kufanya hivyo.

Kwenye mchezo huo Norwich City ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa nyota wake Teemu Pukki katika dakika ya 21, lakini Pierre Aubameyang akasawazisha dakika ya 29, huku Todd Cantwell akipachika bao la pili ila Aubameyang akisawazisha tena kwa mkwaju wa penalti.

Ljungberg amechukua nafasi hiyo kutoka kwa Unai Emery, wiki iliopita, hivyo amedai bado ni mapema sana ila anaamini kuna mambo makubwa yanakuja kutoka kwake kikubwa ni kumuamini.

Huo ulikuwa ni mchezo wa sita kwa Arsenal kushindwa kupata ushindi Ligi Kuu, hivyo kwa sasa wanashika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi kwa pointi 19 ambapo ni pointi saba kufikia nafasi nne za juu.

“Nina uhakika wa asilimia 100 kwamba Arsenal tuna nafasi ya kuingia nafasi nne za juu. Timu zinapoteza pointi kila siku, tunapoteza pointi na wao wanapoteza pointi, hivyo kuna uwezekano wa kuongeza pointi na kupanda nafasi za juu.

“Ninaijua Arsenal na nimekuwa hapa kwa kipindi kirefu, hivyo nina uzoefu, kikubwa ambacho natakiwa kukifanya ni kuwaamini wachezaji wangu na wao kuonesha ushirikiano na mwisho wa siku kila kitu kitaonekana,” alisema kocha huyo.

Ljungberg ni kocha wa muda, lakini wapo makocha wengi ambao wanatajwa kuwindwa kwa ajili ya kuchukua nafasi ya kudumu ambao ni Brendan Rodgers, Mikel Arteta, Patrick Vieira, Max Allegri, Nuno Espirito Santo, Mauricio Pochettino na Carlo Ancelotti.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,455FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles