27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, November 7, 2024

Contact us: [email protected]

Wabunge watakiwa kupewa elimu ya Covid 19

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

 MWANZONI mwa mwezi huu Tanzania ilianza zoezi la kutoa chanjo ya Virusi vya Corona kwa ngazi ya Taifa,baada ya zoezi hilo kuzinduliwa rasmi na Rais Samia Suluhu Hassan.

Kampeni hiyo ya kitaifa ilianza kwa kutolewa chanjo kwa makundi yaliyopewa kipaumbele yakijumuisha watumishi wa afya,viongozi wa dini na waandishi wa habari.

Watu wamekuwa wakiendelea kujitokeza katijka vituo mbalimbali ambavyo vimetambuliwa na serikali kwa ajili ya kutoa huduma hiyo.

Mwitikio wa watu wengine ikiwamo wa tabaka la juu umetajwa kuchangiwa na kujiridhisha kwamba kuna umuhimu wa kupata chanjo ili kuweza kufanya shughuli zao ikiwamo za kiuchumi kwa uhuru.

Mbali na kuendelea kutolewa kwa chanjo hiyo katika vituo mbalimbali hapa nchini,Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Wazee na watoto kwa kushirikiana na wadau wa afya wamekuwa wakitoa elimu kwa makundi mbalimbali huku kukifanyika mijadala.

Hivi karibuni kulifanyika mdahalo wa kitaifa kuhusu Covid -19, uliofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar Es Salaam.

Akichangia mada katika mdahalo huo, Mbunge wa Viti Maalum kupitia kundi la asasi za kiraia (NGO’s),Neema Lugangira,anasema wabunge wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanafanikisha nia ya Serikali katika kulinda wananchi wake na magonjwa ya mlipuko ikiwa ni pamoja na kutoa elimu.

Aidha Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Wazee,Jinsia na Watoto kwa kushirikiana na wadau wengine wa afya wameombwa kutoa elimu kwa kundi la wabunge ili waweze kutoa elimu kwa wananchi hao.

Amesema  ukosefu wa elimu kwa wabunge unaweza kusababisha watu wengine kushindwa kuchanjwa kwa hiari yao hivyo wanahitaji elimu sahihi.

“Lazima tufanye hamasa kubwa sana kwenye jamii,ni lazima tutoe elimu sahihi kwenye jamii,wakati mwingine tunashindwa kuwajibu kwa sababu hatujapatiwa elimu inayotuwezesha kujibu kwa usahihi ili tusiwe sehemu ya kupotosha au kujibu kile ambacho tunadhani ili nasi tusije tukageuka wabobezi wa afya waliosoma kwenye vyuo vya whatsapp,google au vinginevyo,”

“Naomba nitumie fursa hii kuomba sana ,kundi la wabunge ni kundi muhimu na sisi kama wabunge ni nafasi yetu kuwa sehemu ya historia  ya kumuunga mkono Rais mwanamke wa kwanza,katika kufanikisha adhma  yake ya utekelezaji wa chanjo ya Covid -19,”

Amesema wabunge ni moja ya makundi ambayo hayajapatiwa elimu juu cha chanjo ya Covid-19 na kuwa wao ndiyo wahusika moja kwa moja katika kutoa elimu kwa jamii kuhusu chanjo hiyo na kuwatoa hofu juu ya usalama wao.

“Sote tunafahamu chanjo ni hiari sawa lakini nafasi yetu kama wabunge hatupaswi kutumia hiari yetu ya chanjo kuwakosesha wengine hiari yao ya chanjo,na ili tuweze kufanya hivyo mtusaidie mtupe elimu sahihi,”

“Ni lazima tufanye hamasa kubwa kwenye jamii,lazima tutoe elimu sahihi kwenye jamii,nimeona na naomba nipongeze Wizara ya Afya na wadau wa afya mmekuwa mkitoa semina mafunzo mbalimbali kwa makundi maalum ikiwemo viongozi wa  dini,”

“Lengo thabiti kwamba wale watakapokuwa na uelewa sahihi na wao pia wataenda kuelimisha jamii na hii itasaidia kufifisha hii dhana potofu inayoendelea katika jamii yetu.Kwa unyenyekevu mkubwa naomba nikumbushe mmesahau kundi moja muhimu,kundi hili ni sisi wabunge ambao ndiyo wawakilishi wa wananchi,”

Mbunge huyo anasema kirusi cha Covid 19 kimekuwa kikiendelea kujibadilisha na kila kinavyobadilika kinazidi kuwa hatari,hali hii ikapelekea wabobezi wa afya duniani ya kupunguza madhara hayo ni kupitia chanjo.

“Kwa kuwa Tanzania siyo kisiwa nasi pia iilikuwa muhimu kwa kupitia wataalam wetu wa afya  kutathmini mwenendo wa hili wimbi la tatu la Covid 19 na kutoa mwelekeo sisi twende vipi,nimpongeze Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea chanjo ya Covid 19,”

Anasema kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani(WHO),inapokuja chanjo huwa yanatokea makundi matatu ambapo la kwanza ni la wale ambao hata waambiwe nini wanakwenda kuchanja,la pili ni ambao hawataki kuchanja na la tatu ambalo lina watu wengi ni ambao hawajaamua kuchanja kwa sababu hawajaamua.

“WHO inatuambia inapokuja chanjo yapo makundi matatu la kwanza ni lile hata useme nini wanakwenda kuchanja,kundi la pili ambalo wao hata uwambie nini hawataki kuchanja lakini kundi la tatu lipo ambalo ni wengi zaidi wao bado hawajaamua kama wachanje au wasichanje kwa hiyo ningependa kushauri  kwamba hebu tuweke nguvu zaidi kwenye hili kundi la tatu,”

“Tusipoteze  nguvu sana kwenye hili kundi ambalo wanapinga kwa sababu ni wachache,tuweke nguvu kwenye kundi la tatu kwani wanataka kuchanja lakini  bado wana maswali,wanajiuliza,tujitahidi ili hata lile kundi dogo wanaopinga wasiweze kupotosha,”anasema na kuongeza

“Tukifanya hivyo tutakuwa tumeliwezesha kundi kubwa ambalo halijaamua kuweza wenyewe kuchuja na kubaini upotoshwaji,hii itatusaidia kuwaepuka wale wabobezi na wataalam wa mitandaoni maana wanazua taharuki wakati ni upotoshaji,”

Naye Mbunge wa Viti Maalum wanawake Mkoa wa Dodoma,Mariam Ditopile alitoa wito kwa viongozi wa dini,wanasiasa na watu wenye ushawishi mkubwa katika jamii kuwa mstari wa mbele kuhamasisha wananchi juu ya umuhimu wa chanjo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles