23.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 27, 2023

Contact us: [email protected]

Liwiti wahamasishwa kushiriki sensa, anwani za makazi

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Liwiti, Ignas Maembe, amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa viongozi watakaopita katika maeneo yao kwa uwekaji anwani za makazi na kujiandaa kikamilifu kushiriki sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti mwaka huu.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Liwiti, Ignas Maembe (Kushoto), akishiriki mbio na vijana wa jogging zilizokuwa na lengo la kuhamasisha wananchi kushiriki katika zoezi la anwani za makazi na sensa.

Maembe ametoa wito huo leo Machi 27, 2022 wakati wa mazoezi yaliyokuwa na lengo la kuhamasisha wananchi kushiriki katika zoezi la anwani za makazi na sensa.

Amesema uwekaji anwani za makazi utasaidia kutambua nyumba zote zilizopo Liwiti na kwamba sensa itasadia Serikali kupata takwimu sahihi zitakazoiwezesha kupanga vema maendeleo.

“Suala la anwani za makazi na sensa yamekuwa ni ajenda katika vikao vyetu vya maendeleo, tumeshapewa maelekezo na Serikali hivyo ni jukumu langu kuwahamasisha watu washiriki kikamilifu. Sensa ni kwa ajili ya maendeleo yetu na itasaidia Serikali kupanga bajeti itakayoendana na mahitaji ya watu,” amesema Maembe.

Naye Mwenyekiti wa Kikundi cha New Rada Jogging kilichopo Mtaa wa Amani Kata ya Liwiti, Paulo Mtambo, amesema vijana wanapaswa kuwa na mwenendo mzuri ili waweze kujumuika na jamii katika masuala mbalimbali ya maendeleo.

“Michezo inatuunganisha katika mambo mengi tumekuwa tukishiriki katika shughuli za kijamii kama vile kufanya usafi na tayari tumejipanga kuhamasisha wananchi wajitokeze kushiriki kwa wingi katika miradi inayoendelea ya anwani za makazi na sensa,” amesema Mtambo.

Kwa upande wake Polisi Kata wa Liwiti Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Athumani Said, amewataka vijana kuongeza bidii kwenye masomo na michezo na kuepuka makundi ya uhalifu.

Mazoezi hayo yalihusisha vijana kutoka klabu mbalimbali ambao walikimbia kilomita 10 huku wakipita kuhamasisha wananchi kujitokeza kuhesabiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,729FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles