24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

LIVERPOOL YAPEWA HOFFENHEIM MTOANO UEFA

Liverpool, England
KLABU ya Liverpool imepangwa dhidi ya Hoffenheim ya Ujerumani katika droo iliyochezeshwa jana ya michezo ya mtoano ya kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Droo hiyo iliyochezwa mjini Nyon Switzerland, timu ya Celtic itavaana na FC Astana ya nchini Kazakhstan.
Mchezo wa kwanza utaanza Agosti 15 hadi 16 na mchezo wa marudio ni Agosti 22 hadi 23.
Liverpool huenda wakawa na wakati mzuri kutokana na faida ya uwanja wa nyumbani katika mchezo wa kwanza huku Celtic ikianzia ugenini dhidi ya Astana FC.
Hata hivyo, bado Klopp atakuwa katika wakati mgumu kuhakikisha kikosi chake kinaondoka na ushindi kwenye mchezo huo.
Vijana wa Brendan Rodgers, watalazimika kusafiri umbali wa maili 8,000 kufika mji wa Kazakhstan kucheza mchezo wao wa kwanza.
Wakati huo kikosi cha Klopp kikikwepa kukutana na nyota wa zamani wa timu hiyo, Mario Balotelli, ambaye timu yake ya Nice imepangwa kukutana na Napoli.
Kwa mara ya kwanza katika historia ya Hoffenheim, watakuwa wakicheza kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kufanya vizuri kwenye Ligi Kuu ya Ujerumni msimu uliopita.
Wajerumani hao walimaliza ligi hiyo wakiwa nafasi ya nne katika msimu ambao ulikuwa bora kwao, wakimaliza na tofauti ya pointi mbili dhidi ya Borussia Dortmund.
Mfungaji wao mahiri, Andrej Kramaric, ni miongoni mwa wachezaji walioweka rekodi ya usajili baada ya kuhamia klabu ya Leicester City hata hivyo ameshindwa kuonesha makeke yake katika Ligi Kuu England baada ya kufunga mabao 15 alipokuwa Ligi ya Ujerumani, Bundesliga.
Liverpool wakijiandaa na mchezo wao, watalazimika kuwa makini kutokana na ubora wa wapinzani wao, msimu uliopita Hoffenheim walimaliza ligi hiyo bila kupoteza mchezo katika uwanja wa nyumbani wakishinda michezo 11 na kutoka sare michezo sita.
Timu itakayofanikiwa kufuzu katika michezo hiyo ya mtoano itachukua kitita cha pauni milioni 50 na kuingia katika hatua ya makundi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles