25 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Liverpool wamebakisha pointi 27 kuwa bingwa

Liverpool, England

BAADA ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Wolves juzi, vinara wa Ligi Kuu England, Liverpool wamebakisha pointi 27 ili waweze kutangaza ubingwa msimu huu, hivyo wanatakiwa kushinda michezo tisha.

Hadi sasa timu hiyo haijapoteza mchezo hata mmoja tangu kuanza kwa msimu huu kwenye michuano mbalimbali, hivyo kuwa na matumaini makubwa ya kutwaa ubingwa.

Liverpool imeandika historia msimu huu ya kuwa klabu ya pekee ambayo haijafungwa tofauti na klabu zingine za ligi kubwa tano barani Ulaya kama vile England, Italia, Hispania, Ufaransa na Ujerumani.

Rekodi hiyo iliwahi kuwekwa na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England, Manchester City katika msimu wa 2017-18, ambapo walimaliza wakiwa na jumla ya pointi 100, ikiwa ni mara ya kwanza kwa Ligi ya England kwa bingwa kuwa na pointi nyingi kiasi hicho.

Kama wataendelea kushinda michezo yao hiyo tisha hadi kutwaa ubingwa, basi watakwenda kuutangaza ubingwa huo kwenye mchezo dhidi ya Manchester City, Aprili 4, katika Uwanja wa Etihad.

Wakicheza mchezo huo dhidi ya Manchester City, Liverpool watakuwa wamebakisha michezo sita hadi kumalizika kwa Ligi. Mwaka 2001, klabu ya Manchester United ilifanikiwa kutangaza ubingwa Aprili 14 huku zikiwa imebaki michezo mitano.

Hivyo kama Liverpool watafanikiwa kuchukua taji hilo Aprili 4 kwenye mchezo dhidi ya Manchester City, basi itakuwa klabu ya kwanza kutangaza ubingwa mapema katika historia ya Ligi hiyo.

Timu ya Manchester City na Leicester City ndio pekee ambao walipewa nafasi kubwa ya kupambana na Liverpool katika kuwania taji hilo, lakini kama watapoteza michezo yao wiki hii wataifanya Liverpool kujiweka pazuri zaidi.

Liverpool ambao ndio vinara wa Ligi hiyo wana jumla ya pointi 67 baada ya kucheza michezo 23, wakati huo Man City wakishika nafasi ya pili wakiwa na pointi 51 na Leicester City nafasi ya tatu na pointi 48.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,538FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles