25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Liverpool, Man United hapatoshi EPL leo

LIVERPOOL, ENGLAND

VINARA wa Ligi Kuu England, Liverpool leo watakuwa na shughuli pevu ya kusaka pointi tatu dhidi ya Manchester United katika mchezo wa ligi hiyo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Anfield, jijini Liverpool.

Liverpool itashuka dimbani kuwakabili Mashetani hao Wekundu, ikiwa  kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo na pointi zao 61 walizovuna baada ya kucheza michezo 21, wakishinda 20 na kutoka sare mmoja.

Vijana hao kocha Jurgen Klopp wapo katika kiwango bora kwa sasa baada ya kucheza michezo 38 ya ligi bila kupoteza tangu msimu uliopita iliposhindwa kunyakua taji la Ligi Kuu kwa pointi moja mbele ya Manchester City.

United inashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 43 baada ya kucheza michezo 22,ikishinda tisa, sare saba na kupoteza sita.

Kikosi hicho cha United kitashuka kuikabili Liverpool kikitoka kuvuna ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Norwich katika mchezo wao wa ligi uliopita uliochezwa Uwanja wa Old Trafford.

Licha ya ubora wa Liverpool kwa sasa, United itaendelea kujivunia rekodi zao nzuri dhidi ya Majogoo hao wa jiji, kwani katika michezo mitano ya mwisho kuzikutanisha timu hizo, United imeshinda mara moja, Liver mara moja, huku mitatu ikimalizika kwa sare.

Mara ya mwisho United ilipokutana na Liver katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa ligi msimu huu, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1, katikamechi iliyopigwa Old Trafford.

Liverpool iikiwa nyumbani, ilipata ushindi wake wa mwisho dhidi ya United Disemba mwaka juzi , ambapo iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 na kupelekea kocha, Jose Mourinho kutimuliwa.

United ilipata ushindi wake wa mwisho katika Uwanja wa Anfield Januari 17, mwaka 2016, ambapo ilivuna ushindi wa bao 1-0, katika mchezo wa ligi.

Kuelekea mchezo huo, United  huenda ikakosa huduma ya Luke Shaw, Eric Bailly, huku Paul Pogba, Marcos Rojo na  Scott McTominay watakuwa nje ya uwanja wakiuguza majeraha.

Kocha wa United, Ole Gunnar  Solskjaer hakuna uhakika kama straika wake namba moja ndani ya kikosi hicho, Marcus Rashford atakuwa fiti kwa asilimia 100  kucheza mchezo huo, baada ya kuumia katika mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Wolves.

Klopp kwa upande wake, atakuwa akichekelea urejeo wa nyota wake, Joel Matip na Fabinho waliokuwa nje kwa kipindi kutokana na kukabiliwa na majeraha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles