23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

Liverpool haikamatiki Ligi Kuu England

SHEFFIELD, ENGLAND

KINARA wa Ligi Kuu England, Liverpool imeendelea kugawa vichapo kwenye ligi hiyo baada ya kuicharaza Sheffield United  bao 1-0 katika mchezo uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Bramall Lane, jijini, Sheffield.

Bao ya Liverpool lilitupiwa kambani na  kiungo Mdachi, Georginio Wijnaldum dakika ya 70.

Ushindi huo unaifanya Liverpool kuzidi kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 21 baada ya kushinda michezo yao saba ya waliyoshuka dimbani hadi sasa,.

Kipigo hicho kinaikiacha kikosi cha Sheffield katika nafasi ya 10 ikiwa na pointi nane baada ya kucheza michezo saba, ikishinda miwili, sare miwili na kupoteza mitatu.

Licha ya kupata ushindi huo, lakini vijana hao wa Jurgen Klop walitapa tabu hasa mbele Sheffield ambayo ilionekana kucheza kimkakati zaidi kwa muda mwingi wa mchezo.

Sheffield United ilianza mchezo huo kwa kuisoma Liverpool,ikiziba mianya yote, lakini ikitumia mashambulizi ya kushtukiza kusaka mabao.

Hali hiyo ilifanya dakika 45 za kipindi cha kwanza kumalizika bila timu hizo kufungana,licha ya Liverpool kumiliki mpira zaidi, lakini ukuta wa Sheffield ulikuwa imara.

Liverpool ilirudi kwa kasi zaidi kipindi cha pili ikionekana wazi kuja na mpango wa kusaka mabao ili kuibuka na ushindi katika mchezo huo.

Hata hivyo, Ukuta wa Sheffield ulikuwa kikwazo kwa washambuliaji wa Liverpool, Saido Mane, Mohammed Salah na Roberto Firmino kutokana na kukosa maarifa ya kuupangua na kufunga mabao.

Wijnaldum alipeleka kilio kwa wenyeji kwa kuifungia Liverpool dakika ya 70 kwa shuti kali akimalizia mpira uliookolewa na mabeki wa Sheffield na kumkuta katika eneo zuri.

Bao hilo liliifanya Liverpool kuzidisha  mashambulizi lango ni mwa Sheffield,lakini Salah alipoteza nafasi ya wazi ya kufunga bao la pili dakika ya 77 akiwa yeye na mlinda mlango wa Sheffield,Dean Henderson.

Naye, Leon Clarke wa Sheffield atabidi kujilaumu mwenye kutokana na nafasi nzuri aliyoipata, lakini alishindwa kuisawazishia timu yake na kujikuta akipiga mpira uliopaa juu ya lango la Liverpool.

Jitihada za Sheffield kutafuta bao la kusawazisha zilishindwa kuzaa matunda na kujikuta hadi  90 za mtanange huo zinakamilika Liverpool ikifanikiwa kuondoka kifua mbele na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji wao.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,460FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles