LISSU RASMI PICHANI…

Hatimaye Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu leo ameonekana hadharani katika baadhi ya picha zilizotumwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Katika picha hizo, Lissu anaonekana amenawiri na akiwa na afya njema na tabasamu huku akipunga mkono kama ishara ya kusalimia akiwa na watu mbalimbali na nyingine akiwa peke yake amekaa katika kiti cha magurudumu (wheelchair) na nyingine akiwa amelala kitandani.

Jana akiwa katika mkutano na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe pamoja na mambo mengine aliahidi kutoa picha na video zinazomuonyesha Lissu alivyo sasa baada ya kupigwa risasi na matibabu anayoendelea nayo nchini Kenya.

Lissu ambaye alipigwa risasi Septemba 7, mwaka huu mkoani Dodoma na watu wasiojulikana, amekuwa jijini kwa zaidi ya siku 40 akitibiwa majeraha ya risasi alizopigwa ambapo amefanyiwa upasuaji mara 17 na anatarajiwa kupelekwa nje kwa matibabu zaidi mwishoni mwa mwezi huu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here