LISSU NJE KWA DHAMANA

0
530

Hatimaye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Julai 27, imemwachia huru kwa dhamana Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Lissu ameachiwa baada ya kutimiza masharti ya dhamana, yaliyomtaka kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh milioni 10 kila mmoja na haruhusiwi kutoka nje ya Dar es Salaam isipokuwa kwa kibali cha mahakama.

Kesi hiyo imetajwa mapema asubuhi ambapo Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, alitoa masharti hayo na kuahirisha kesi kwa muda wa nusu saa ili kutoa nafasi kwa wadhamini ambao walizuiwa nje ya mahakama kutokana na watuhumiwa wa kesi nyingine ya ugaidi kufikishwa mahakamani hapo ambapo watu waliondolewa na wengine kuzuiwa kuingia kwa sababu za kiusalama.

Lissu anatuhumiwa kwa makosa ya uchochezi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here