20.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 28, 2022

LISSU: NIMELALA NYUMBANI BAADA YA MIEZI 11

Na MWANDISHI WETU


MBUNGE wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema),  amesema kwa mara ya kwanza amelala nyumbani kwake jana baada ya kukaa hospitalini kwa miezi 11.

Lissu alishambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 akiwa nje ya makazi yake mjini Dodoma Septemba 7 mwaka jana na baadaye kukimbizwa katika Hospitali ya Nairobi  Kenya, kabla ya kupelekwa Ubelgiji kwa matibabu zaidi, Januari 6 mwaka huu.

Jana, Lissu aliandika katika mitandao ya  jamii akisema:  “Kwa mara nyingine nawaleteeni habari njema. Alfajiri ya January 6 ya mwaka huu, niliondoka Nairobi Hospitali na kusafiri hadi Leuven, Ubelgiji kwa ajili ya matibabu zaidi.

“Jana (juzi) Agosti 6, mwaka huu ilikuwa mwezi wa saba kamili tangu niletwe hapa Ubelgiji kwa ajili hiyo.

“Leo (jana) Agosti 7 ni miezi 11 to the day niliposhambuliwa na watu wanaojulikana sana kama ‘watu wasiojulikana. Septemba 7, mwaka jana, sikulala nyumbani kwangu. Tarehe 7 Agosti ya leo (jana), miezi 11 kamili baadaye, nimeamkia nyumbani kwangu.

“Tarehe 7, Septemba iliyopita wote mlikuwa na hofu kubwa kama ningemaliza siku hiyo, au siku chache zilizofuata, nikiwa hai.

“Miezi 11 kamili baadaye, Professor Dk. Wilhelmus Jan Mertsemakers, daktari wangu tangu nilipokuja University Hospital Leuven, amesema sina sababu ya utabibu ya kuendelea kukaa hospitalini.

“Prof. Mertsemakers amesema nitaendelea na uponyaji nikiwa nyumbani kwangu. Nitatembelewa na homecare nurses kila siku nyumbani kuniangalia naendeleaje. Na nitarudi hospitali kumwona kila baada ya wiki mbili.

“Bado nina lichuma kubwa kwenye paja liko kama antenna ya TV za mwaka ’47. Na Prof. Mertsemakers amesema nitakaa nalo kwa si chini ya miezi sita. Lakini habari ya mujini ndiyo hiyo; nimetoka hospitalini.

“Hongereni sana kwa kazi nzuri ya kuniuguza na kuniponya. Na chochote mtakachokula au kunywa siku ya leo (jana) mnibakishie. Siko mbali,” aliandika Lissu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,097FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles