26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Lissu: Nikishinda nitaunda baraza la mawaziri 15

 UPENDO MOSHA – MOSHI 

MGOMBEA wa urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema), Tundu Lisu amesema iwapo atashinda nafasi hiyo, atahakikisha anauanda baraza la mawaziri wasiozidi 15. 

Pia aliahidi kutengeneza mfumo utakaowezesha kuwa na uhuru wa vyombo vya habari, ikiwemo kufuta mfumo wa uchujaji wa habari. 

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Moshi mkoani Kilimanjaro jana, Lissu alisema ili kupunguza gharama za uendeshaji wa Serikali, atahakikisha baraza lake linakuwa na watu wachache. 

“Nitakuwa na baraza dogo, nitafuta baadhi za wizara kama Wizara ya Habari… haina kazi zaidi ya kupeana ulaji, lina vitu vitu vingi na mzigo tu kwa walipa kodi,” alisema Lissu. 

Kuhusu suala la uhuru wa vyombo vya habari, alisema ilani ya Chadema imezungumzia uhuru, haki na maendeleo ya watu ambao wanapaswa kuwa huru kusema lolote, ikiwemo waandishi kuandika habari zao.

“Kwangu hakutakuwa na kesi za uchochezi, haya makosa yanayodhibiti watu kusema na kuandika tutayaondoa, tutatumia mfumo wa nchi ya Ghana, hatutakuwa na uchujaji wa habari. 

“Mfumo huu uliojengeka kwa zaidi ya miaka 60 haukidhi tena mahitaji yetu, wafanyabiashara ni kilio, wakulima, wafanyakazi na kila mtu kwa sababu Serikali hii, na mfumo uliopo haukidhi mahitaji ya nchi,” alisema Lissu. 

Akizungumzia kupitisha muda wa kufanya mkutano mjini Moshi, Lissu alisema hakufanya mkutano, baada ya kufika alichofanya ni kutoa salamu kisha kuondoka. 

Alisema Mkoa wa Kilimanjaro amefanikiwa kufanya mikutano mikubwa ya hadhara eneo la Kamwanga na Tarakea na kwamba atarudi tena mkoani humo baada ya wiki tatu au mbili. 

“Tumeahirisha mkutano huu, ratiba ya Tume inaonyesha Oktoba 6 nilitakiwa kuwa Moshi, tutarejea baada ya wiki tatu au mbili, tunahitaji wananchi watafakari kazi waliyoifanya jana (Juzi), tukija tutaanzia Moshi mjini,” alisema Lissu. 

Alisema Jimbo la Hai lina siku yake pekee ya kimkakati kutokana na mgombea ubunge wake, Freeman Mbowe yupo maeneo mengine akisaidia wagombea wengine. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles