LISSU NGOMA NZITO, WAKILI WAKE AOMBA APELEKWE MAHAKAMANI

0
654

WAKILI wa Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Fatma Karume amesema anapeleka ombi Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam kuomba mteja wake Tundu Lissu apelekwe mahakamani.

Hatua hiyo imekuja masaa machache baada ya kumtembelea Lissu katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam na kuzuiwa kumuona zaidi ya mara mbili.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya kituo hicho, Fatma amesema ameambiwa na askari aliowakuta kuwa hawatamwachia Lissu kwa sababau upelelezi wa makosa yake ya uchochezi unaendelea na atafikishwa mahakamani baada ya kukamilika kwa upelelezi huo.

Lissu alikamatwa jana jioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam (JNIA), akielekea katika kikao cha halmashauri ya EALS kilichotarajiwa kuanza leo nchini Rwanda.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here