26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Lissu amnadi Ado Shaibu akiwa polisi

Na MWANDISHI WETU-TUNDURU

MGOMBEA urais wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amefanya mkutano wake wa kampeni Tunduru jana akimnadi mgombea ubunge kupitia chama cha ACT-Wazalendo, Ado Shaibu ambaye hata hivyo hakuwepo kwenye mkutano huo kutokana na kuitwa polisi.

Akihutubia umati wa wananchi wa eneo hilo Lissu alirejea kauli zake za mara kwa mara kuhusu haki na uhuru.

“Tunduru mpoooo? aaaah aaah nataka wasikie kule walikompeleka Ado Shaibu.Tunduru mpoooo?”kisha akajibiwa kwa sauti tupooooo!

“Hiyo imekaa vizuri jambo la kwanza watu wa Tunduru Kaskazini mgombea wangu wa ubunge katika jimbo hili ni Ado Shaibu wa ACT-Wazalendo.

“Jambo la pili naomba mfahamu mgombea ubunge wa jimbo hili wa chama changu cha Chadema anaitwa Ado Shaibu” alisema Lissu huku akishangiliwa.

Alisema anazungumza uhuru kwa sababu vile vile kila mmoja amekabwa koo.

“Kwanini wamemkamata Ado Shaibu leo? kwanini kila wakati wanatunyanya? kwasababu hatuna uhuru, ukitaka kusema tofauti na wimbo wa Magufuli wanakukamata hawa waliovaaa uniform au wale wanaoitwa watu wasiojulikana” alisema Lissu huku akishangiliwa.

Alisema katika nchi hii  imekuwa rahisi kumkosa Mungu aliyewaumba kuliko kumkosa Magufuli waliyemchagua kuwa rais.

“Yaani ukianza kuzungumza habari ya Magufuli hapa unaanza kuangalia maaskari wako wapi yaani ni hivi kinyago tumekichonga wenyewe halafu tunakiogopa” alisema Lissu huku akishangiliwa.

Alisema nchi imejaa vitisho na kwamba hata ukiwaangalia maaskari (waliokuwepo kwenye mkutano huo) wanatembea na mabomu.

“Nani kawaambia hapa kuna vita, hatupumui! kwahiyo ndio maana tunazungumza uhuru kwa sababu kila mmoja wetu amekabwa koo, Vyombo vya Habari haviko huru, Bunge haliko huru Masheikh wakizungumza wanakamatwa na kufunguliwa kesi za ugaidi maaskofu wakizungumza wanakamatwa na huyu huyu anayejiita mcha Mungu,” alisema huku akishangaliwa.

Alisema watu wa Tunduru wasije wakasahau kuna zaidi ya masheikh 200 ambao wako katika magereza mbalimbali nchini na kwamba ndio maana anazungumza juu ya haki na uhuru.

“Hakuna haki polisi, mahakamani, ukipeleka mtoto shule nchi imejaa dhuluma…Wafanyakazi wanadhulumiwa, wafanyabiashara wanadhulumiwa hata mapolisi hawa wanadhulumiwa”.

Alirudia tena kauli yake ambayo amekuwa akiisema katika mikutano yake mingi ya kampeni kwamba wafanyakazi wote wa nchi hii hawajalipwa nyongeza ya mishahara kwa miaka mitano ambayo sheria ya Tanzania inasema walipwe kila mwaka.

“Mapolisi, wanajeshi, walimu, magereza manesi wote wamepigwa miaka mitano 

Sasa serikali inayodhulumu hadi hao wanaoilinda ni wa maana gani?,” alihoji Lissu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles