31.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

LISSU AKANA KUCHAPISHA TAARIFA ZA UCHOCHEZI

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (kushoto), akiwa na washtakiwa wenzake katika kesi ya uchochezi, wakitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam jana kusikiliza kesi hiyo.
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (kushoto), akiwa na washtakiwa wenzake katika kesi ya uchochezi, wakitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam jana kusikiliza kesi hiyo.

Na Kulwa Mzee-Dar es Salaam

MBUNGE wa Singinda Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), amedai hakushiriki kuchapisha taarifa‎ za uchochezi zenye kichwa cha habari ‘Machafuko yaja Zanzibar’ kwa sababu yeye si mchapishaji.

Lissu alidai hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, alipokuwa akisomewa maelezo ya awali dhidi ya kesi ya uchochezi inayomkabili pamoja na wahariri wa Gazeti la Mawio.

Mshtakiwa huyo akisomewa maelezo hayo na Wakili wa Serikali, Patrick Mwita, alikubali jina lake, umri wake, kazi na makazi yake na kwamba ameshtakiwa kwa makosa hayo yanayomkabili.

Hata hivyo, Lissu alikana kushiriki kuchapisha taarifa‎ hizo za uchochezi.

“Sikubali kama kulikuwa na uchaguzi halali wala Serikali halali Zanzibar kwa sababu kitu hicho hakipo kisheria,” alidai Lissu mahakamani hapo.

Lissu alikana kuwatisha na kuwatia hofu wananchi wa Zanzibar wasiweze kuingia kwenye marudio ya Uchaguzi Mkuu.

Mhariri wa Gazeti la Mawio, Simon Mkina, Jabir Idrisa na  mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehboob, kwa upande wao walikubali maelezo yao binafsi yakiwamo majina yao, umri na kazi wanazofanya na kuyakana mashtaka yote yanayowakabili.

Washtakiwa wote wanakabiliwa na mashtaka matano, likiwamo la kuandika habari za uchochezi kinyume na sheria ya magazeti ya mwaka 2002.

Inadaiwa kuwa Januari 12 hadi 14, 2016 katika Jiji la Dar es Salaam, washtakiwa watatu; Jabir, Mkina na Lissu, kwa pamoja waliandika na kuchapisha taarifa‎ za uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho ‘Machafuko yaja Zanzibar’.

Wanadaiwa katika shtaka jingine kwamba Januari 14 mwaka jana katika Jiji la Dar es Salaam, walichapisha habari hizo ili kuleta chuki kwa wananchi wa Zanzibar.

Mshtakiwa Mehboob anadaiwa kuwa Januari 13 mwaka jana katika jengo la Jamana lililopo Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam, alichapisha gazeti la Mawio lililokuwa na taarifa za uchochezi.

Inadaiwa kuwa mshtakiwa huyo pia alichapisha gazeti hilo bila ya kuwasilisha hati ya sheria ya kiapo kwa Msajili wa Magazeti.

Mbali na mashtaka hayo, washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kuwa Januari 14, mwaka jana jijini Dar es Salaam, bila ya kuwa na mamlaka yoyote, waliwatisha na kuwatia hofu wananchi wa Zanzibar wasiweze kuingia kwenye marudio ya Uchaguzi Mkuu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles