LISSU AKAMATWA UWANJA WA NDEGE DAR AKIELEKEA RWANDA

0
683

MWANASHERIA Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu amekamatwa na Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam saa 12 jioni leo Julai 20, katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere akijiandaa kuelekea nchini Kigali.

Hata hivyo, Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene amethibitisha kukamatwa kwa Lissu lakini haijulikani anashikiliwa katika kituo gani.

Taarifa za kukamatwa kwake zilisambaa muda mfupi ambapo baada ya kukamatwa aliandika ujumbe wa maneno wa kuwataarifu wanachama wenzake uliosomeka kuwa:

“Council members. I’m at the airport getting ready to fly to Kigali for the EALS Governing Council meeting slated for tomorrow. Persons introducing themselves as police officers from ZCO’s office in Dar have come to arrest me and are taking me to the Central Police Station for interrogation. Please notify everyone concerned.” From Lissu’s.

(Wajumbe  wa halmashauri, nipo Uwanja wa ndege najiandaa kuelekea Kigali kwenye kikao cha halmashauri ya EALS kinachoanza kesho.  Watu waliojitambulisha kama maofisa kutoka ofisi ya ZCO Dar es Salaam, wamekuja kunikamata na kunipeleka Kituo cha kikuu cha Polisi).

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam, Lucas Mkondya ameliambia Mtanzania Digital kuwa kesho asubuhi atatoa taarifa kama Jeshi la Polisi linamshikilia Lissu au la.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here