Lil Wayne kuachia albamu ya mazishi

0
838

New York, Marekani

RAPA Lil Wayne, amewaambia mashabiki zake wakae tayari kwa ujio wa albamu yake mpya inayojulikana kwa jina la mzishi.

Msanii huyo alitumia ukurasa wake wa Instagram na Twitter kwa kuposti video fupi akieleza kuwa, albamu hiyo imekamilika na kilichobaki ni kuiachia.

Hata hivyo hakuweka wazi kuwa ni lini ataizindua. “Muda mfupi albamu ya mazishi itakuwa mtaani, hivyo mashabiki wakae tayari kuipokea,” alisema msanii huyo huku akiposti pamoja na jeneza.

Mapema mwezi huu msanii huyo alikutana na maswali ya mashabiki zake ambao walikuwa wanataka kujua lini albamu hiyo ataiachia, hivyo aliwajibu kuwa ataiachia mapema Februari.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here