23.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Lil Wayne anusurika kifo Atlanta

BADI MCHOMOLO NA MITANDAO
KIONGOZI wa kundi la Young Money, Lil Wayne, juzi alinusurika kifo alipokuwa Atlanta, nchini Marekani, baada ya basi alilopanda kupigwa risasi na watu wasiojulikana.
Lil Wayne alikuwa katika mzunguko wa maonyesho yake ya muziki katika mji huo, huku akitumia basi lililokuwa likiwabeba baadhi ya wasanii wa kundi lake.
Hata hivyo, katika shambulio hilo la risasi hakuna mtu aliyejeruhiwa. Kupitia mtandao wa Twitter, msanii huyo aliandika kwamba ameshangaa kuona gari hilo likishambuliwa kwa risasi, lakini anashukuru hakuna aliyejeruhiwa.
“Ni jambo la hatari kwa maisha ya binadamu, tunashukuru hakuna mtu aliyeumia kutokana na shambulizi hilo, Mungu alitulinda na tutaendelea kumuomba atulinde zaidi katika shoo zetu kama tulivyozipanga katika ratiba.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles