23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Lijualikali: Hata mimi nimeitoa mbali Chadema

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

MBUNGE wa Kilombero, Peter Lijualikali (Chadema), amezidi kuanika namna ambavyo wabunge wa chama hicho wamekuwa wakikatwa fedha zao na kisha kuzuiliwa kuhoji matumizi yake huku akieleza kuwa hatishwi na kauli za kwamba chama hicho kimemtoa mbali kwani hata yeye amekitoa mbali tu.

Hivi karibuni mbunge huyo ameingia kwenye malumbano na chama chake baada ya kuamua kubaki na msimamo wake wa kushiriki vikao vya Bunge wakati Chadema ilipotoa maelekezo kwa wabunge wake kutoingia bungeni ili wakae karantini siku 14 kujikinga na corona.

Akizugumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki Dar es Salaam, Lijualikali alisema kuwa baada ya kuelezea namna ambavyo wanakatwa fedha, kuna baadhi ya wabunge wa chama hicho wamekuwa wakidai kwamba wanaotoa malalamiko kwenye kukatwa mishahara yao wanapotosha.

“Sakata la wabunge kukatwa au kuchangia chama sisi hatukatai wala hatupingi, unapaswa kuchangia chama na hatupingi kabisa.

“Katika katiba ni kweli inaelezea wabunge kuchangia chama. Sawa katiba inasema kila mbunge anachangia kwa ujenzi wa chama ni kweli na nakubali ndio maana nilikuwa natoa, lakini huchangii kitu ambacho hakina matokeo, bali unachangia kwa kujua nini ambacho kinakwenda kufanyika, ndo maana hata wananchi wanapolipa kodi wanajua kodi yao inakwenda kununua dawa, kujenga shule, hospitali, hivyo unapochangia lazima ujue, sio unatoa tu fedha zako halafu huna haki ya kujua zimetumikaje au hata kuhoji namna ambavyo zimetumika. 

“Hakuna utawala wa sheria na hakuna demokrasia hapo, kwa hiyo sisi tunakubali tulikuwa tuna wajibu wa kulipa fedha kwenye chama asilimia 20, hata hivyo lazima tujue fedha hizi zinafanya kazi gani. 

“Ndiyo tunahoji hapa, wengine wanasema mbona CAG (Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali) hajaona, CAG haingii kwenye vikao vya chama na wala kujua tuliambiwa nini,” alisema Lijualikali.

Alisema kuwa CAG anachoangalia ni kile kilichomo kwenye makaratasi, na sisi tunazungumza tulichokubaliana kwenye vikao, kama CAG anakuaga anauliza, hakuja kwenye vikao vya wabunge wakati mwenyekiti anatujaza.

“Halafu watu wengi hawajui. Hivi ni wana Chadema wangapi wanajua akaunti mama zote za chama kuwa mwamba ndiyo anayetia saini ikiwemo akaunti ya fedha za ruzuku,” alisema Lijualikali. 

Aliongeza kuwa akaunti za Chadema wanaotia saini ni Mwenyekiti Freeman Mbowe, Katibu Mkuu, Mkurugenzi wa Fedha na mtu mwingine kutoka Bodi ya Wadhamini.

 “Mwamba ni mwenyekiti wa chama, ndiyo anakaa pale juu. Mwamba huyu huyu ndiyo anayeteua Katibu Mkuu wake ambaye naye ni mtia saini katika akaunti, halafu mwamba huyu kwa kukaa na katibu mkuu ndiyo wanakaa kushauriana kuteua Mkurugenzi wa Fedha ambaye pia ni mtia saini, na mwamba mwenyewe naye anatia saini, hesabu za kazi hizi. 

“Na hesabu iko hivi, Mwenyekiti (Mwamba), Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha ndio pesa yao hiyo. Wawili wanaweza kusaini kuchukua mzigo (fedha). Hivi mimi ni diwani pale tuna akaunti ya kata yetu, utaratibu hauruhusu kabisa diwani kuwa mtia saini, utaratibu huo haupo.

“Hakuna waziri ambaye ni mtia saini wa akaunti za wizara, hakuna hata akaunti moja ambayo Rais Dk. John Magufuli na hata marais waliopita wanatia saini. Lakini huku kwetu huku mwamba ndiyo mtia saini na ndio maana watu wanasema ni Saccos, kwa hiyo sehemu zote zinazopigwa za hela jamaa ndio anasaini na wenzake halafu mzigo unatoka, kwa hiyo sisi, yaani mimi Lijualikali ambaye nilikuwa jela ninachangia hela kwenye chama, nilifungwa jela miezi sita na nimekaa ndani miezi mitatu, kila mwezi nilikuwa nachangia.

“Watu wa mwamba hawakuwahi kutoa hata Sh 100 mpaka leo, yaani Peter Msigwa na timu yake, na kama wanabisha tumuombe Spika atoe vielelezo kama ataona inafaa,” alidai Lijualikali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles