24 C
Dar es Salaam
Thursday, July 25, 2024

Contact us: [email protected]

Ligi Kuu Bara vita kuripuka upya leo

Winfrida Mtoi

LIGI Kuu Tanzania Bara, msimu wa 2019/20 unatarajia kuanza leo kwa michezo mitano kupigwa kwenye viwanja tofauti, timu mpya zikiwa ni Namungo FC na Polisi Tanzania.

Katika mechi hizo, Namungo watakuwa nyumbani kuwakaribisha jirani zao Ndanda FC Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi, wakati Polisi Tanzania wataikaribisha Coastal Union dimba la Ushirika Moshi.

Namungo inayonolewa na kocha Mrundi, Hitimana Thierry, inatarajia kuvutia wapenzi wengi wa soka mkoani humo, kutokana na kusheheni nyota wenye majina akiwemo Adam Salamba, Paul Bukaba na Mohammed Ibrahim, ambao msimu uliopita walikipiga Simba.

Kwa upande wa Polisi Tanzania, ni kikosi kinachoundwa na wachezaji wengi wenye uzoefu na Ligi Kuu, wakiwemo Ditram Nchimbi, Marcel Kaheza na Pato Ngonyani.

Michezo mingine, Mbao FC wataumana na Alliance  Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, dimba Sokoine jijini Mbeya, ndugu wawili Tanzania Prisons watapimana ubavu na Mbeya City, Biashara United itachuana na Kagera Sugar, Uwanja wa Karume, Mara.

Kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi anatarajia kuwa kivutio kwa wapenzi wengi wa soka, baada ya kurejea kikosini humo.

Ligi hiyo itaendelea kesho kwa michezo miwili, Lipuli FC itakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar, Uwanja wa Samora, Iringa, wakati Singida United itakuwa ugenini kuikabili Mwadui Uwanja Kambarage, Shinyanga

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles