30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

LHRC yampa tano mbunge Hawa Mchafu

*Yasema ndiye pekee anejua kutumia fursa za kituo hicho

Na Gustafu Haule, Pwani

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimemtaja mbunge wa viti maalum mkoa wa Pwania, Hawa Mchafu kuwa ndiye pekee nchini anayejua kutumia fursa mbalimbali zinazotolewa na kituo chake.

Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Wakili Anna Henga akiwasikiliza wajasiriamali kabla ya kuanza kutoa mafunzo ya uendelezaji biashara zao kwa njia ya kidigitali Wilaya Bagamoyo.

Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi wa kituo hicho, Wakili Anna Henga Machi 2, mwaka huu wakati akizungumza na Wanawake wajasiriamali zaidi ya 300 waliokutana katika viwanja vya Mwanakalenge vilivyopo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani kwa ajili ya kupata mafunzo ya uendelezaji wa biashara zao kwa njia ya kidigitali yaliyoratibiwa na mbunge huyo kwa ufadhili wa LHRC.

Amesema LHRC chake kimekuwa kikitoa msaada wa kisheria kwa jamii ikiwemo masuala ya unyanyasaji wa kijinsia,ukatili,masuala ya miradhi na hata mafunzo mbalimbali ya kuwajengea uwezo Wanawake wajasiriamali.

Amesema katika kuchangamkia fursa hizo ameona mbunge Hawa ndiye amekuwa akijitoa na kutumia fursa hizo vizuri hususan katika kuwasaidia wanawake wajasiriamali.

Henga ameongeza kuwa mbunge huyo amekuwa akiandika maandiko mbalimbali na kuyafikisha kituoni hapo kwa ajili ya kuomba ufadhili wa mafunzo ya kuwasaidia wanawake  na kwakutambua umuhimu huo wamekuwa wakimkubalia kwakuwa yanatija kubwa kwa wanawake.

“Kwa kweli leo tumekutana hapa kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wanawake wajasiriamali wa Bagamoyo kuhusu uendelezaji wa biashara Kidigitali na matumizi ya teknolojia lakini kazi kubwa imefanywa na Hawa kwa kuwa ndiye aliyeratibu,”amesema Henga.

Amesema wajasiriamali wa Mkoa wa Pwani wanapaswa kuona fahari ya kuwa na mbunge mwenye juhudi kubwa za kuwapigania huku akisema LHRC itaendelea kushirikiana na mbunge huyo kwa kila hitaji lenye maslahi ya wanawake.

Kwa upande wake hawa ameishukuru LHRC kupitia mkurugenzi huyo kwakufanyakazi nzuri ya kuwakomboa Wanawake nchini Tanzania .

Mchafu,amesema LHRC imekuwa ikitoa mafunzo mbalimbali kwa wabunge yakiwemo mafunzo ya sheria ili kupanua wigo wa kusaidia jamii inayokumbwa na changamoto katika maeneo yao.

Amesema baada ya kuifahamu vizuri LHRC na kufahamu fursa zao ndipo alipowiwa kuomba kwa kuandika maandiko juu ya kuomba ufadhili wa mafunzo ya masuala ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia .

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mafunzo hayo, Mohamed Usinga amesema LHRC imefanya kazi kubwa kutoa mafunzo hayo na kwamba wao wataendelea kutoa mikopo ya wanawake hao kwa tija.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles