26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, August 14, 2022

Lewis aomba kurudia pambano na Tyson

NEW YORK, MAREKANI

BINGWA wa zamani wa ngumi za uzito wa juu duniani, Lennox Lewis, ameweka wazi kuwa yupo tayari kurudi ulingoni kupambana na mpinzani wake, Mike Tyson, endapo atawekewa mezani kitita cha dola milioni 100, zaidi ya Sh bilioni 234 za Kitanzania.

Bingwa huyo mara tatu wa heavyweight, aliwahi kupambana na Tyson na kufanikiwa kushinda kwa KO katika raundi ya nane huko mjini Memphis mwaka 2002.

Pambano hilo liliacha historia kubwa katika ngumi kutokana na ubora wa wapiganaji hao, hivyo tangu hapo hawajawahi kupigana tena, sasa Lewis amedai yupo tayari kupigana na mpinzani huyo mwenye historia kubwa.

Lewis mwenye umri wa miaka 53 sasa, baada ya kushinda pambano hilo mwaka 2002, alirudi tena ulingoni Juni 2003 na kufanikiwa kushinda pambano lake dhidi ya Vitali Klitschko na likawa pambano lake la mwisho kabla ya kutangaza kustaafu.

Wakati huo Tyson mwenye umri wa miaka 52 kwa sasa, baada ya kukubali kichapo hicho, alirudi tena ulingoni mara tatu kabla ya kuja kutangaza kustaafu mwaka 2005.

Tangu wawili hao wastaafu ngumi hadi sasa hakuna ambaye kati yao ameweza kurudi ulingoni kwa ajili ya pambano la kulipwa, hivyo wakifikia makubaliano tunaweza kuwaona tena wakipigana.

“Naomba nitumie nafasi hii kila mmoja ajue kwamba, ninaweza nikaweka pembeni kustaafu kwangu na nikarudi ulingoni kwa kitita cha dola milioni 100, kama Tyson atakuwa tayari basi fedha ziwekwe mezani nirudi kupambana naye,” alisema Lewis.

Hata hivyo, bingwa huyo alikumbushia sababu zilizomfanya ashinde katika pambano lake dhidi ya Tyson mwaka 2002.

“Kabla ya pambano hilo, nilijaribu kuangalia historia ya Tyson, nikaona wazi kuwa historia yake inafanana na yangu, hivyo niliamua kufanya mazoezi ya nguvu zaidi yake ili niweze kushinda na nikafanikiwa kufanya hivyo,” aliongeza.

Hata hivyo, baada ya Lewis kutoa kauli hiyo, Tyson hadi sasa hajaweka wazi kama yupo tayari kurudi ulingoni kwa kitita hicho cha fedha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,656FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles