28.7 C
Dar es Salaam
Monday, October 25, 2021

LESOTHO YAIOMBA KENYA MSAADA KUREKEBISHA KATIBA

NAIROBI, KENYA

SERIKALI ya Lesotho imeomba msaada wa ushauri kutoka Kenya ili kuufanyia mageuzi mfumo wa utawala wa Serikali yake iweze kusitisha misukosuko ya kisiasa nchini humo.

Ujumbe wa nchi hiyo, ukiongozwa na Waziri Mkuu Mothetjoa Metsing, ulikutana na Naibu Rais William Ruto ofisini kwake Karen juzi.

Ulisema kwamba Lesotho imeanzisha mpango wa kuandika katiba mpya.

Metsing, ambaye aliandamana na Waziri wa Biashara, Joshua Setipa na Balozi wa Lesotho nchini hapa, Nyolosi Mphala, alisema nchi yake imeamua iwe na katiba mpya kabla uchaguzi kufanyika baadaye mwaka huu.

“Tumekuja hapa kuomba usaidizi wa kufanya mabadiliko nchini mwetu ili kusitisha siasa zinazotikisa utulivu, ambazo zinashuhudia kufanyika kwa uchaguzi wa mara kwa mara.

“Tulikuwa na uchaguzi wa ghafla mwaka uliopita na mwaka huu tena tutakuwa na uchaguzi mwingine,” alisema Metsing.

Alisema mabadiliko wanayolenga yamenuia kuleta maelewano ya kugawa mamlaka na kuhakikisha mizozo yoyote inayohusu uongozi inatatuliwa kikamilifu.

Metsing alisema siasa za usaliti na kuhamahama kutoka chama kimoja hadi kingine ndizo chanzo cha chaguzi kufanyika kila mara.

“Tuna matatizo, wabunge huamua kuhamia vyama tofauti kila mara wanapokosana kuhusu masuala tofauti. Hii imesababisha chaguzi zisizotarajiwa,” alisema.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,099FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles