25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

LeRoy ajiuzulu kuifundisha Congo Brazzaville

Claude-Leroy-talks141015BBP720BRAZZAVILLE, CONGO

KOCHA raia wa nchini Ufaransa, Claude LeRoy, aliyekuwa mkufunzi wa kikosi cha timu ya taifa ya Congo Brazzaville, amejiuzulu kuifundisha timu hiyo.

LeRoy, mwenye umri wa miaka 67, aliuambia uongozi wa soka wa timu kwamba anatarajia kuacha kuifundisha timu hiyo kutokana na kubanwa na majukumu mengine.

Hivyo kocha huyo ameamua kufanya maamuzi hayo mara baada ya kuiongoza timu hiyo kuingia hatua ya makundi ya kusaka tiketi ya kombe la dunia baada ya kuifunga Ethiopia mabao 2-1.

Kumekuwa na tetesi kwamba huenda kocha huyo akarudi kuifundisha timu ya taifa ya Cameroon, ambayo imemtimua kocha wake, Volker Finke kutokana na matokeo mabaya ya timu hiyo.

LeRoy ana historia kubwa ya kuwa kocha aliyeshiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mara nane na akifanikiwa kutwaa taji hilo mwaka 1988, akiwa na kikosi hicho cha Cameroon.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles