24.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Leicester kuwapa mashabiki wake zawadi ya Krismasi?

CHELSEA'S MANAGER RANIERI LOOKS AT THE CROWD AFTER ENGLISH PREMIER LEAGUE SOCCER MATCH AGAINST LEEDS IN ...ADAM MKWEPU NA MITANDAO

KOCHA wa vinara wa Ligi Kuu England, Leicester City, Claudio Ranieri, ana mtihani mgumu leo pale timu yake itakapoikabili Everton kwenye moja ya michezo ya Ligi Kuu England.

Ushindi wa Leicester City utakua zawadi tosha kwa mashabiki wake kuelekea Sikukuu ya Krismasi kwani watakua wamejihakikishia timu yao kukaa kileleni mwa ligi wakati wa sherehe hizo.

Leicester City inajitupa uwanjani baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya mabingwa watetezi wa ligi, Chelsea, mchezo ambao ulipelekea kocha wa Chelsea, Jose Mourinho, kufungashiwa virago.

Washambuliaji, Riyad Mahrez pamoja na Jamie Vardy, wameonekana kuwa na mvuto wa kipekee pamoja na kumpa imani kocha wao baada ya Vardy kufunga mabao 15 huku akitabiriwa kufunga zaidi ya mabao 18 msimu huu.

Wasiwasi upo juu ya klabu ya Everton kama inaweza kuiondoa Leicester City kileleni kabla ya Krismasi na hii ni endapo ama Arsenal au Manchester City wakishinda michezo yao.

Kocha wa Everton, Javier Martinez, anakiri kwamba ikiwa kama klabu inaongozwa na bajeti ndogo inaweza kusababisha matokeo ya mshangao kwa wapenda soka.

Martinez alidai Leicester City inastahili kuwa nafasi waliyonayo sasa kutokana na kujipanga vema baada ya kugundua mapungufu yao kabla ya kuingia ligi kuu.

Ranieri anatamani wachezaji wake kufanya jitihada za kutafuta ushindi katika mechi hiyo kwa kuwa anafahamu si rahisi kuifunga timu hiyo.

Everton haikufungwa katika mechi nane ilizocheza katika michuano yote lakini wameweza kupata pointi tatu katika michezo miwili ya mwisho kati ya sita walizocheza.

Kumbukumbu zinaonesha kwamba klabu ya Leicester City inakuwa katika wakati mgumu inapokutana na Everton kwasababu kati ya mechi 20 walizowahi kucheza, walifanikiwa kushinda moja tu.

Ingawa katika kumbukumbu hizo timu hiyo haikuwahi kufungwa katika michezo 11 waliyocheza nyumbani ambayo walifanikiwa kushinda saba kati ya hizo.

Martinez alithibitisha mlinzi wa klabu hiyo, John Stones, atacheza mechi hiyo baada ya kukosa mchezo dhidi ya Norwich City kutokana na kuwa majeruhi.

Southampton vs Tottenham

Baada ya klabu zote kuambulia kichapo wiki iliyopita, hivyo matumaini yao yamekuwa katika mchezo huu ambao utawafanya kurudisha hari ya mchezo.

Spurs chini ya Mauricio Pochettino ilifungwa 2-1 na Newcastle United na ni dhahiri wamepania kushinda mchezo wa leo ili kutinga ‘top four’.

Southampton nao pia wamekuwa wakipata matokeo mabovu katika mechi za hivi karibuni na timu hiyo inayofundishwa na Ronald Koeman haina budi kushinda kufufua matumaini yao kucheza michuano ya Ulaya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles