24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Lebanon inavyopambana na ndoa za utotoni

OthmanMiraji, Ujerumani

KUTOKANA na uchunguzi wa kuaminika ni kwamba inakisiwa watoto milioni 15 duniani huozeshwa kwa lazima kila mwaka. Asilimia 80 kati yao ni wasichana. Katika Afrika chini ya Jangwa la Sahara na barani Asia idadi ya wasichana wanaokutana na janga hilo ni kubwa mno. Nchini Niger robo tatu ya wasichana huozeshwa wakiwa chini ya umri wa miaka 18.

Katika Jamhuri ya Afrika ya Kati ni asilimia 68, Chad asilimia 67 na Bangladesh niasilimia 59. Huko India idadi ya wasichana wa aina hiyo imepungua sana mnamomiaka 25 iliyopita, kutoka 50 hadi 27 asilimia.

Miaka14, 15, 16: katika umri huo wasichana huozeshwa nchini Lebanon. Lakini sasa wanaharakati katika nchi hiyo ya Kiarabu wanaendesha kampeni kubwa ya kuitokomeza mbali tabia hiyo. Kwa mfano,msichana Basma (jina nimelibadilisha), mwenye umri wa miaka 14, alikataah katakata kuolewa, licha ya kwamba wazee wake walishikilia afungishwe ndoa. Hata hivyo, makaratasi ya kufungandoa  yalikusanywa na sherehe ndogo ilifanywa, bila ya msichana mwenyewe kutoa kauli ya kukubali. Bwana arusiambaye ni Binamu wa Basma alikabidhiwa mkewe.

Lakini Basma alikataa kabisa kufanya tendo la ndoa na badala yake aliigeukia Jumuiyaya kutoa Msaada, Himaya (Ulinzi). Jumuiya hiyo ilimtuma mfanyakazi wake  aende kuwa wazee wa Basma ili wabadilishe msimamo wao. Lakini aligongamwamba. Wazee hao walikaza kamba na kushikilia Basma lazima aolewe na binamuwake, hata kama Bi. Arusi huyo mtarajiwa hataki. Himaya ilimtuma mwanasheriawake akaitetee kadhia ya Basma mahakamani. Cha kusikitisha ni kwamba hakimualimwambia wakili wa Basma kwamba Mimi sina la kufanya katika suala hilo.Katika ndoa hiyo ni familia na mamlaka za dini ndizo zilizo na dhamana.  Mwishowe ndoa ya Basma ilibidi iidhinishwe.

Haijulikani hasa idadi ya wasichana wanaofikwa na msiba kama huo nchini Lebanon. Lakini niwengi sana. Hakuna tarakimu rasmi zinazochapishwa. Katika uchunguzi wa maoni yawatu uliochapishwa  Septemba, mwaka huu na Jumuiya ya Wanawake ya RDFL ni kwamba asilimia tisa ya wanaume na wanawake walioulizwa walikiri kwamba waliozeshwa wakiwa wangali bado watoto. Idadi yawasichana walioozeshwa wakiwa watoto ilikuwa kubwa zaidi kuliko ile yawavulana. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwasaidia watoto (UNICEF), kutokanana tarakimu zake za mwaka 2009 ni kwamba asilimia sita ya wasichanahulazimishwa kuolewa wakiwa bado hawajafikia umri wa miaka 18.

Ndoa za watoto si kinyume na sheria katika nchi hiyo. Hakuna sheria inayoweka umriwa kuanzia kwa mtu kuoa au kuolewa. Pia hakuna sheria ya aina moja kwa wanawake wanaoolewa. Kuna sheria ya familia inayotumika kwa kila moja ya jamii za kidini darzeni moja za nchi hiyo. Mtu yeyote anayeolewa au kuoa huko Lebanon hawezi kumkwepa padri, askofu au kadhi. Kwa Wakristo wa nchi hiyo umri wa kuruhusiwa kuolewani si chini ya miaka 14  na kwa Waislamuunaanzia punde baada ya msichana kuvunja ungo, yaani kutokwa na damu yake ya mwanzo ya mwezi.

Licha ya hayo, Walebanon wengi wanaupinga mtindo huu wa kuozesha watoto, ikiwa ni wasichana au wavulana. Utafiti uliofanywa na Jumuiya ya RDFL umekuja na matokeoya kushangaza. Asilimia 84 ya watu walioulizwa walisema wanapinga  kufungwa ndoa kwa mtu aliye chini ya umri wamiaka 18. Zaidi ya hayo, watu hao wote walikubaliana kwamba umri wa mtukufungishwa ndoa uwe kutoka miaka 18 na zaidi. Ni wazi  kwamba ndoa za utotoni haziungwi mkono kabisana watu walioulizwa na ambao walikuwa chini ya umri wa miaka 35.

Kunatofauti baina ya nadharia na mazoea katika suala la ndoa huko Lebanon. Kwabaadhi ya watu mila hutiliwa sana maanani. Mara nyingi watoto huozeshwa kwalazima kutokana na sababu za kifedha. Wazee huvutiwa na fedha za mahari auzawadi wanazopewa kwa kuwashawishi sana watoto wao wakubali kuingia katikandoa. Nchini humo ndoa za watoto zimeenea miongoni mwa wakimbizi wa Syriawaliokwenda kutafuta hifadhi tangu mwaka 2011. Uchunguzi uliofanywa na Shirikala Umoja wa Mataifa la Wakaazi Duniani umekuja na matokeo ya kutisha, nayo nikwamba huko Lebanon katika kila wasichana wanne wa Kisyria, mmoja basi ameolewa akiwa kati ya umri wa miaka 15 hadi 17. Kuna nambari maalum ya simu ambayo inawatangaza wasichana au wavulana wa umri huo ambao wazee wao  wako tayari kuwaoza.

Watu wengi nchini humo walistuka hapo mwisho wa Oktoba mwaka huu walipoliona tangazo ndani ya mtandao wa kijamii lililosema:  Bi. Arusi Bikira, zikioneshwa picha zawasichana wanaotaka kuozeshwa wakiwa na umri wa miaka 12,13,14,15, mtuyeyote  aliyepiga nambari ya simu iliyooneshwa juu angeweza kupatiwa maelezo zaidi kuhusu wasichana hao.

Mada hii ya ndoa za utotoni inachemka hivi sasa. Malalamiko mengi yanatolewa ndani ya mitandao ya kijamii. Wanaharakati wa Jumuiya ya RDFL wanaendesha kampeni ya kuwaamsha watu juu ya hatari ya hali hiyo. Mfano ni msichana Faidia  (jina nimelibadilisha) aliyekuwa na umri wa miaka 15. Yeye inasemakana alijiua baada ya kutoa mimba ya mtoto wake wa kwanza. Sababu ya kuozeshwa akiwa bado ni mtoto ni umaskini na hali ngumu ya maisha. Harakati zinazofanywa na Jumuiya ya RDFL zinaambatana na sheria na ni halali.  Mafanikio yamepatikana.  Si tu watu wameanza kuamka kimawazo, lakini kampeni hiyo imeliwekea mbinyo Bunge la Lebanon. Kwa miaka sasa kumekuwapo Muswada wa sheria unaotaka umri wa kuoa au kuolewa usiwe chini ya miaka 18.  Lakini haifikiriwi kwamba muswada huo utapitishwa karibuni uwe sheria kamili.

Pia katika nchi zinazoitwa zimeendelea mtindo wa ndoa za utotoni uko. Nchini Marekani kuna mikoa 25 ambako hakuna kiwango cha umri wa chini kwa msichanakuolewa kisheria. Hapa Ujerumani ninakoishi ziko pia ndoa za utotoni, hasamiongoni mwa watu waliohamia nchini. Mwaka 2016 idadi yao ilifikia 1500,japokuwa sasa inapungua. Wengi wa watu hao wametokea Syria, Bulgaria naUgiriki. Sheria ya mwaka 2017 ilikataza wasichana kuolewa chini ya umri wamiaka 16, na ikatangaza kwamba ndoa zao hazita kubaliwa. Na ikiwa wakati wakufunga ndoa umri wa mmoja wa wafunga ndoa ni baina ya miaka 16 na 18, mahakamandio itakayotoa uamuzi kama ndoa hiyo ibatilishwe.

Kihistoria ndoa za utotoni zilikuwa ni jambo la kawaida. Hoja iliyotolewa kuunga mkono mtindo huo ni kwamba watu walikufa mapema, kwa hivyo ndoa za aina hiyo zilikuwa zinachukuliwa ni njia barabara ya kuibakisha idadi ya watu kuwa juu. Zamani ilikuwa ni kawaida kwa wasichana kuchumbiwa hata kabla ya kubaleghe.

Katika Uyunani ya zamani ndoa za mapema na wasichana kuzaa yalikuwa mambo ya kawaida. Hata wavulana wakiwa umri wa miaka 12 na 15. Dini kadhaa zinakataza mtu kuoa au kuolewa kabla ya umri wa kubaleghe.  Katika nchi kadhaa hata wavulana huozeshwa wakiwa bado ni watoto.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles