Lava Lava awafunga mdomo wabaya wake

0
997

GLORY MLAY

MSANII wa muziki kutoka lebo ya WCB, Abdul Iddi maarufu kwa jina la Lava Lava, amewafunga midomo wanaedai kuwa anaishi kwenye nyumba ya mpenzi wake.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Lava Lava alisema maisha ya uhusiano ni siri na makubaliano baina ya watu wawili hivyo anawashanga watu wanaomsema vibaya kwa kuishi nyumbani kwa mpenzi wake.

“Kwanza tunapunguza majukumu, hata hivyo ninanyumba ya kuishi, hivyo kwenda kukaa kwake wiki, mwezi sioni tatizo kwa sababu ni mpenzi wangu, shida ni kwamba watu wengi wamezoea kuona mwanamke ndio anayepaswa kuishi kwa mwanamke, sio kweli.

“Watu wanatakiwa kubadilisha mawazo yao, maisha yamebadilika hayapo kama zamani,” alisema msanii huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here