30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 19, 2021

Laurence Badibe ana jambo lake kwa mashabiki

TOOWOOMBA, AUSTRALIA


MWIMBAJI mahiri wa gospo nchini Australia, Pastor Laurence Badibe, ameweka wazi kuwa baada ya wimbo, Tobinela Roi Jesus, kufanya vizuri Ulaya, Marekani na Canada sasa ni zamu ya Afrika.


Akizungumza na MTANZANIA, Badibe alisema wimbo huo wenye ujumbe wa kuishaiwhi jamii kumwimbia na kumtukuza Mungu, umefanyika baraka kwa watu wa matifaifa mbalimbali hivyo anatamani mashabiki zake wa Afrika Mashariki waisikilize na kutazama video hiyo.


“Nimepokea simu nyingi kutoka huko Ulaya, Marekani, Canada na hapa Australia watu wakinipongeza kwa kazi nzuri. Natamani pia wimbo huu uwafikie mashabiki hapo Afrika, video tayari ipo kwenye chaneli yangu ya YouTube, nimemshirikisha Chiza Musenge na ipo kwenye mahadhi ya Rhumba, naomba sapoti kutoka kwa mtu yeyote,” alisema mwimbaji huyo mwenye asili ya Kisangani, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,848FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles