31.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 3, 2024

Contact us: [email protected]

LATRA CCC, FCS kulinda haki za watumiaji usafiri

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri wa Ardhini kutoka LATRA kwa kushirikiana na Shirika la Asasi za Kiraia nchini (FCS), wamesaini mkataba wa makubaliano ya miaka mitatu ya programu itakayowezesha kulindwa kwa haki za mtumiaji wa barabara, reli na waya.

Akizungumza Oktoba 22,2024 wakati wa kusaini makubaliano hayo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa FCS, Justice Rutenge, amesema ushirikiano huo ni muhimu katika kuchechemua uwakilishi wa wananchi na kuimarisha mifumo ya ulinzi wa watumiaji.

“Kujitolea kwetu kwa ulinzi wa watumiaji kunatokana na dhana ya msingi ya haki muhimu za watumiaji, ikiwa ni pamoja na haki ya malipo ya madai, elimu ya udhibiti wa usafirishaji wa bidhaa na huduma za ardhini,” amesema Rutenge.

Amesema LATRA CCC ni mdau muhimu wa maendeleo ya ulinzi wa watumiaji katika sekta ya usafiri wa nchi kavu, hivyo kupitia ushirikiano huo FCS itaongeza ujuzi wa kujenga uwezo wa kutekeleza mipango inayolenga kulinda haki za watumiaji nchini.

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa LATRA CCC, Daud Daud, amesisisitiza umuhimu wa ufumbuzi wa changamoto na ushirikiano miongoni mwa wadau wa maendeleo wakati Tanzania inaelekea kukuza mazingira yanayounga mkono haki za mlaji.

“Ushirikiano kati yetu ni mfano wa juhudi za pamoja za kukuza mazingira ya biashara ya usawa na kuwawezesha watumiaji ujuzi kutambua haki zao na chaguzi sahihi za usaidizi.” Amesema Daud.

Naye Mkuu wa Programu FCS, Nasim Losai, amesema ushirikiano huo utaongeza chachu ya kutambulika zaidi majukumu ya LATRA CCC kwa jamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles