Lanie: Filamu za Tanzania zina sauti mbaya

Lanie
Rashid Lanie

 

NA FESTO POLEA, ZANZIBAR

PRODYUZA wa muziki kutoka Afrika Kusini aliyeandaa muziki katika filamu ya Kalushi, Rashid Lanie, ameshangazwa na tabia za baadhi ya watengeneza filamu za Tanzania kutumia miziki ya filamu mbalimbali badala ya kutengeneza za kwao.

Lanie alisema katika filamu za Tanzania alizoziona, amegundua mapungufu makubwa katika muziki, akidai kwamba filamu nyingi zimetumia muziki wa wanamuziki kutoka filamu nyingine, jambo ambalo litaendelea kudumaza filamu za Tanzania.

“Nimeona baadhi ya filamu za Tanzania, nimegundua wana uwezo mkubwa wa kuigiza na picha si mbaya sana, lakini sauti wanazoweka katika filamu hizo ni mbaya na zinakera unapotazama filamu zao,” alisema.

Aliongeza kwamba muziki unaotumika katika filamu, unatakiwa utumike kwa kutengenezwa na wataalamu wanaojua sauti ya muziki na si kuchukua tu sauti ama muziki ilimradi wakati wapo maprodyuza wenye uwezo mzuri lakini hawatumiki ipasavyo,” alisema.

Lanie aliongeza kwamba muziki aliotengeneza kwa ajili ya ‘Kalushi’, iliyofungua pazia la filamu katika tamasha la Ziff mwaka huu, aliutengeneza akiwa na hisia za filamu baada ya kuletewa ili aiweke sauti, hivyo ndivyo inavyotakiwa si kuchukua sauti ilimradi tu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here