24.6 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

Lampard awaweka kikao mastaa Chelsea

LONDON, ENGLAND

BAADA ya timu ya Chelsea kulazimishwa sare dhidi ya Leicester City kwenye mchezo wa Ligi Kuu England mwishoni mwa wiki iliopita, kocha wa timu hiyo Frank Lampard, aitisha kikao na mastaa wa timu hiyo na kuwataka kuonesha thamani yao kwenye michezo inayofuata.

Mchezo huo ambao ulipigwa juzi, Chelsea walikuwa wa kwanza kupata bao dakika za mapema kupitia kwa mchezaji wao Mason Mount, lakini nyota wa Leicester City, Wilfried Ndidi aliweza kuisawazishia timu yake na kuufanya mchezo huo umalizike kwa sare ya bao 1-1 huku Chelsea wakiwa kwenye uwanja wa nyumbani Stamford Bridge.

Huo ulikuwa ni mchezo wa tatu mfululizo kwa Lampard kukosa ushindi baada ya kuchezea kichapo cha mabao 4-0 kwenye mchezo wa dhidi ya Man United, kabla ya kufungwa na Liverpool kwenye fainali ya Uefa Super Cup na juzi kutoa sare.

“Sare sio matokeo mabaya, wachezaji wangu wameonesha tayari wamerudi uwanjani, lakini kulikuwa na changamoto kwa baadhi ya wachezaji kushindwa kuonesha kiwango chao, kuna wakati wachezaji walitakiwa kuwa imara ili kuuweza mchezo huo.

“Tunatakiwa kuutawala mchezo, hatukufanikiwa kwa kiasi kikubwa kuutawala mchezo, lakini ninaamini tunajua wapi tulikosea na lazima tuyafanyie kazi.

“Timu inatakiwa ionekane ikicheza, inatakiwa ionekane ikimiliki mpira dhidi ya wapinzani, hapo itakuwa kazi rahisi kufanya vizuri, kwa sasa tunatakiwa kuangalia mchezo unaofuata ili kupata matokeo,” alisema Lampard.

Mbali na kutoka sare, lakini kocha huyo alikuwa na mapokezi makubwa kwenye uwanja huo ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu ajiunge na timu hiyo wakati huu wa kiangazi.

“Ilikuwa siku muhimu sana kwangu hasa kutokana na mapokezi niliyoyapata kutoka kwa mashabiki wa nyumbani, awali nilikuwa kama mchezaji na sasa nimerudi kama kocha, ninajua nina deni kwa mashabiki ambao wanahitaji kuona timu yao ikishinda na nina uongozi ambao ndoto zao ni mataji, hivyo ninaamini tutafanikiwa, ninawashukuru mashabiki kwa sapoti yao,” aliongeza kocha huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles