24.3 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Laini milioni 19 zasajiliwa alama za vidole

Asha Bani, Dar es Salaam

Serikali imesema hadi sasa imefanikiwa kusajili laini milioni 19.681.086 kwa alama za vidole ambayo ni sawa na asilimia 42 zinazomilikiwa na watu mil 7.6 ikiwa zimebaki siku 18 zoezi hilo lifikie tamati.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), James Kilaba alipokua wakielezea hali ya usajili wa laini za simu za mkononi kwa njia ya alama za vidole kuanzia Mei Mosi mwaka huu hadi Desemba 13 mwaka huu.
Kilaba amesema pia idadi ya laini ambazo wamiliki wana namba za utambulisho za NIDA (NIN) lakini hawajasajili kwa njia ya alama za vidole ni milioni 5.599.610 ambazo zinamilikiwa na takribani watu milioni tatu.
“Laini za simu zisizosajiliwa kwa alama za vidole ni milioni 21.782 .906 ambazo zinamilikiwa na takribani watu milioni 10.5,” amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dk. Arnold Kihaule amesisitiza kasi ya uandikishaji NIDA kwani kuna manufaa mengi huku akisema idadi ya watu wasiopata vitambulisho au namba za NIDA na kwamba hawafanyi lolote zaidi ya milioni tatu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,455FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles