Lady Jaydee, Dully Sykes majaji wapya Bongo Star Search

0
1362

JEREMIA ERNEST

Wakongwe wa muziki wa Bongo Fleva Abul Sykes ‘Dully Sykes’ na Judith Wambura ‘Lady Jaydee’  wameteuliwa kuwa miongoni mwa jopo la majaji watakaokuwa katika shindano la kusaka vipaji la Bongo Star Search (BSS) msimu wa 10.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Septemba 17, katika uzinduzi wa msimu huu mpya Jaji Mkuu wa shindano hilo, Rita Poulsen ‘Madam Rita’ amesema mwaka huu wamekuja kivingine na majaji wapya.

“Mwaka huu ni msimu wa 10 bado tunafanya hili shindano mengi tumepitia hadi kufika hapa.

“Mwaka huu katika safu ya majaji tutakuwa na wakongwe wa muziki hapa nchini ambao ni Dully Sykes na Komando Lady Jaydee na kwa mwaka huu hatutakuwa na jaji aliyezoeleka kwa muda mrefu Salama Jabir kutokana na shughuli anayoifanya pia mtangazaji wetu atakuwa ni mchekeshaji Idris Sultan,” amesema.

Madam Rita amesema usahili mwaka huu utafanyika Mwanza, Arusha, Dodoma, Mbeya na Dar es salaam ambapo mchakato mzima utaonyeshwa kupitia channel ya Swahili katika king’amuzi cha StarTimes.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here