28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

LADY JAY DEE AWACHANA WAPENDA SIFA

Na JENNIFER ULLEMBO

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura ‘Lady Jay Dee’, amesema ni vema waimbaji wanaofanikisha nyimbo mbalimbali za wasanii wengine wakapewa sifa na kupongezwa.

Jay Dee ambaye hivi karibuni ameachia wimbo wake mpya uliopewa jina la ‘I miss You’, alisema imekuwa ni tabia kwa baadhi ya wasanii kushindwa kuweka wazi nyimbo zao wanazotoa zimefanikishwa na nani.

“Mimi tabia hiyo sina na vizuri wengine wakatambua wanavyofanya si vizuri, unapopewa ushirikiano na msanii mwingine iwe ni kwa kuandikiwa mashairi au kitu chochote, useme na kumpa sifa kwa kile alichokufanyia.

“Wengi wana tabia ya kujisifia na kusimama mbele za watu kueleza kuwa wamefanya kazi zao wenyewe, wakati nyuma kuna mkono wa mtu mwingine,” alisema Lady Jay Dee.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,307FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles