25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, December 9, 2023

Contact us: [email protected]

Lady Gaga akamatwa na polisi

Lady Gaga
Lady Gaga

MALIBU, CALIFORNIA

MSANII mwenye vituko nchini Marekani, Stefani Germanotta ‘Lady Gaga’, juzi alikamatwa na polisi kwa kosa la kuendesha gari ambalo halina namba ya usajili.

Msanii huyo alikutwa mitaani akiwa na gari lake lenye rangi nyekundu aina ya Pick Up Truck, huku likiwa halina namba mbele na upande wa nyuma.

Hata hivyo, msanii huyo baada ya kufikishwa kituo cha polisi aliwaonesha kadi ya gari hilo na kuwaambia kwamba ni gari mpya, hivyo bado hajapewa namba.

Polisi walichukua leseni ya msanii huyo na kumtaka afuatilie kwanza suala la namba ya gari hilo kwa ajili ya kukwepa usumbufu.

Baada ya muda msanii huyo kupitia akaunti yake ya instagram alisema kwamba anashukuru kurudishiwa leseni yake wakati anaendelea kufuatilia namba yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles