UONGOZI wa Ligi Kuu Hispania, La Liga umesema utatuma ripoti kwa kamati ya Serikali inayohusika na kupambana na uhalifu ya kulaani vitendo vya ubaguzi wa rangi na lugha chafu vilivyofanywa na mashabiki katika mchezo wa Espanyol dhidi ya Barcelona Jumamosi iliyopita.
Kwa mujibu wa tovuti ya ligi hiyo, ripoti hiyo itakuwa ikilaani maneno ya kibaguzi kuelekezwa kwa mshambuliaji wa Barcelona, Neymar Jr pamoja na lugha ya kuudhi dhidi ya klabu hiyo.
Pia Shirikisho la Soka la nchi hiyo kitengo cha nidhamu ilisisitiza kukataza vitendo vya kuchochea vurugu, ubaguzi wa rangi, chuki katika michezo.