Kylie, Scott wataka kurudiana

0
622

KWA mujibu wa E! News, staa wa mitindo kutoka familia ya Kardashian, Kylie Jenner na baba wa mtoto wake Travis Scott, wameanza kuwasiliana kwa ajili ya kutaka kurudiana ikiwa ni wiki mbili tangu wawili hao watangaze kuachana.

Inasemekana kuwa, kila mmoja amekuwa akimkumbuka mwenzake, hivyo wamejikuta wakitumiana ujumbe mfupi wa maandishi wa kutaka wamalize tofauti zao.

“Kila mmoja kati yao anaona hawezi kuishi bila ya mwenzake, wanajikuta kuwa na mawazo kila wakati, hivyo wanataka kumaliza tofauti zao warudi kuishi pamoja, walisema E!News.

Wawili hao tayari wana mtoto wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi nane, lakini walifikia makubaliano ya asilimia 50 kwa 50 kumlea mtoto wao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here