29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

KYLIE MINOGUE: SIOLEWI TENA

CANBERRA, AUSTRALIA


MSANII wa muziki na filamu nchini Australia, Kylie Minogue, ameweka wazi kuwa hana mpango wa kuolewa tena katika maisha yake baada ya kuachana na mume wake Joshua Sasse.

Mrembo huyo amesema kwa sasa kitu ambacho anaweza kukiangalia ni jinsi ya kuweza kuyatengeneza maisha yake mwenyewe na kuuweka sawa mwili wake na kufanya mambo kwa kutumia akili.

Wawili hao walifunga ndoa Februari 2016 na kuja kuachana mwaka uliofuata, hivyo mrembo huyo amesema hawezi kubembeleza mapenzi na hataki kuumiza kichwa kwa ajili ya uhusiano, lakini anataka kuumiza kichwa kwa ajili ya maisha yake.

“Hakuna mtu ambaye anaweza kunibadilisha mawazo yangu kwa sasa, sina mpango tena wa kuingia kwenye uhusiano na kujadili masuala ya ndoa, nadhani hata wazazi wangu hawawezi kunishawishi.

“Kitu kikubwa ambacho ninaweza kukiangalia kwa sasa ni jinsi ya kuendesha maisha yangu mwenyewe, niliweza kuwa mwenyewe kwa miaka mingi na sasa nataka kurudi tena kwenye aina hiyo ya maisha kwa kuwa ndoa zina usumbufu wake na mimi sitaki usumbufu,” alisema Kylie.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles